IQNA

Eneo la Waislamu Ufilipino laadhimisha mwaka wa tatu wa kuanzishwa

15:29 - January 18, 2022
Habari ID: 3474821
TEHRAN (IQNA)- Waislamu katika eneo la Ufilipino lenye mamlaka ya ndani la Bangsamoro wanaadihimisha mwaka wa tatu tokea wapate mamlaka ya dani ya kujitawala.

Eneo hilo ambalo rasmi linakulikana kama Eeneo lenye Mamlaka ya Ndano la Bangsamoro katika Ukanda wa Waislamu Mindanao (BARMM)  limeanzisha sherehe za mwaka wa tatu wa kupata mamlaka ya dani ambapo. Sherehe hizo ambazo zilianza Jumatatu katika Makao ya Serikali ya Bangsamoro mjini Cotabato zinafanyika kwa kuzingatia kanunuzi za kuzuia maambukizi ya Corona.

Nara na kauli mbiu ya sherehe za mwaka huu ni "Kubadilisha Maisha ya Watu, Kuleta Mabadiliko Bangsamoro, Kusherehekea Mafanikio ya Amani na Utawala wa Kimaadili."  Katika kipindi cha miaka mitatu serikali ya Mamlaka Ya Ndani ya Bangsamoro, kumekkuwa na jitihada za kufikia amani kamili, ustawi na mabadiliko.

Ufilipino ni nchi iliyo kwenye eneo la Funguvisiwa la Malay huko kusini-mashariki mwa Asia. Ufilipino ina visiwa 7,641 vinavyohesabiwa katika makundi matatu yanayoitwa kufuatana na ujirani na visiwa vikubwa vya Luzon, Visaya, Mindanao.

Kwa mujibu wa takwimu, idadi ya Waislamu Ufilipino ni zaidi ya milioni 5.1, yaani asilimia 6 ya watu wote wa nchi hiyo. Zaidi ya nusu ya Waislamu wanaishi katika kisiwa cha kusini cha Mindanao.

3477417/

captcha