IQNA

Jinai za Israel

Mchambuzi: Waranti za ICC dhidi ya watenda jinai wa Israel ni za kihistoria

21:21 - November 24, 2024
Habari ID: 3479798
IQNA – Mchambuzi mmoja wa kisiasa nchini Iran amesema waranti au hati za kukamatwa zilizotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) dhidi ya watenda jinai wawili wa Israel ni mabadiliko ya kihistoria katika uga wa kimataifa.

Akizungumza na IQNA, Masoumeh Nasiri ameashiria hatua ya ICC dhidi ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wa zamani wa masuala ya kijeshi Yoav Gallant na kusema mahakama hiyo ina ushahidi wa kutosha kuwahukumu wawili hao kwa makossa ya uhalifu wa kivita.
Wamefanya uhalifu kama vile kutumia njaa kama njia ya vita, uhalifu dhidi ya ubinadamu, mauaji, na vitendo vingine vya kinyama, alibainisha.
Kilicho muhimu ni uamuzi wenyewe, ambao haujawahi kutokea na unaweza kuchukuliwa kuwa hatua ya mabadiliko katika historia ya uhusiano wa kimataifa, ameongeza.
Nasiri amesisitiza kuwa, lolote ambalo limetajwa dhidi ya maafisa hao wawili wa Kizayuni linaweza kufuatiliwa mmoja baada ya jingine.
Uwezekano kwamba wahalifu hao wawili wanaweza kukamatwa katika nchi tofauti ni jambo lingine muhimu, alisema.
Amesisitiza kwamba nchi za Kiislamu zinapaswa kufuatilia kesi dhidi ya Netanyahu na Gallant hadi mwisho ili wazuiliwe na kufunguliwa mashitaka ili mahali popote duniani pasiwe salama kwa wahalifu hao.
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kwa moja, imetaka kutekelezwa mara moja na kwa ukamilifu hukumu ya ICC, amesema.
Mtaalamu huyo aidha amesema uamuzi huo umezua hofu katika mioyo ya maafisa wa Israel na kuufanya ulimwengu kutokuwa salama kwao.
Aliendelea kusema kuwa nchi zinapaswa pia kutoa wito wa kufukuzwa utawala wa Tel Aviv kutoka duru za kimataifa na kuwatenga maafisa wa Israel kutokana na matukio ya michezo, kiutamaduni, kisanii na kitaaluma.
Majaji wa ICC walisema Alhamisi kwamba kulikuwa na "sababu nzuri" za kuamini Netanyahu na Gallant "kwa makusudi na kwa kujua waliwanyima raia katika Gaza vitu ambavyo ni muhimu kwa maisha yao."
Mahakama hiyo pia ilisema watu hao walibeba "dhima ya uhalifu" kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu wakati wa mashambulizi ya umwagaji damu huko Gaza.
Vita vya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza vilivyoanza Oktoba mwaka jana vimesababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina 44,000 wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto na wengine wengi kujeruhiwa.

3490800

Habari zinazohusiana
captcha