Kwa mujibu wa Televisheni ya Al Jazeera, klipu hiyo inamuonyesha Yassin akisoma Qur’ani Tukufi wakiwa na mke wake.
Klipu hiyo imesambazwa katika ukurasa wa Twitter wa Balozi wa Qatar nchini Malaysia Fahad bin Mohammed Kafood. Watumizi wa mitandao ya kijamii wamefurahishwa na klipu hiyo huku wengi wakimuombea duaa za kheria waziri mkuu huyo.