IQNA

Ulimwengu wa Kiislamu

Naibu Waziri Mkuu wa Malaysia auzawadia Msikiti nchini Peru tasfsiri za Qur’ani

18:56 - August 17, 2024
Habari ID: 3479289
IQNA - Naibu Waziri Mkuu wa Malaysia Fadillah Yusof alikabidhi nakala za tafsiri na tarjuma za Qur’ani Tukufu katika Kihispania na Kilatini kwa msikiti mmoja nchini Peru.

Alisema msaada huo utawasaidia kufahamu maana ya aya za  Qur’ani Tukufu, hivyo kurahisisha uelewa na ufundishaji wa Uislamu kwa watu wa Peru.

Yusof, pamoja na ujumbe wa Malaysia na wawakilishi kutoka ubalozi wa Malaysia nchini Peru waliungana na jumuiya ya Waislamu wakati wa sala ya Ijumaa kwenye Msikiti wa Magdalena Del Mar katika mji mkuu wa Peru wa Lima jana.

Alisema kuwa kando ya kuimarisha Ukhuwah (udugu) miongoni mwa Ummah, ziara hiyo inaakisi dhamira ya Malaysia ya kuunga mkono juhudi za kuhubiri Uislamu  nchini Peru na, kwa upana zaidi, Amerika Kusini.

Katika ziara hiyo, alikutana na Rais wa Jumuiya ya Kiislamu ya Lima Murad Hamide na kujadiliana kuhusu kusaidia jamii ya Waislamu katika nchi hiyo ya Amerika Kusini.

Mkuu na wawakilishi wa msikiti huo walionyesha nia yao ya kushirikiana na Malaysia ili kuongeza maarifa, uelewa na umilisi wa Uislamu.

Walitoa wito wa kusaidiwa katika uanzishwaji wa shule ya kimataifa ya Kiislamu na utekelezaji wa viwango vya Halal katika vyakula jambo ambalo litanufaisha jumuiya ya Kiislamu na wafanyabiashara wa ndani nchini Peru, Yusof alisema.

Peru inakadiriwa kuwa na idadi ya watu karibu milioni 34, na takriban Waislamu 5,000.

Jumuiya ya Waislamu nchini Peru kwa kiasi kikubwa inajumuisha wahamiaji kutoka nchi kama vile Lebanon na Palestina, na idadi ndogo ya Waperu asilia ambao wamesilimu.  

3489529

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: malaysia qurani tukufu
captcha