IQNA

Qur'ani na Maisha

Naibu Waziri Mkuu wa Malaysia: Qur'ani ina mfumo wa utawala, maelewano ya kijamii

19:55 - October 11, 2024
Habari ID: 3479573
IQNA - Naibu Waziri Mkuu wa Malaysia Fadillah Yusof amesisitiza umuhimu wa Qur'ani Tukufu kama mfumo elekezi wa utawala, mwenendo wa kibinafsi, na maelewano ya kijamii.


Akizungumza katika Kongamano la Dunia la Qur'ani 2024 huko Kuala Lumpur siku ya Alhamisi, aliangazia kanuni za Qur'ani ambazo hazipitwi na wakati na ambazo pia zinavuka mipaka ya kitamaduni na ya muda.
Qur'ani Tukufu inatoa sio tu mwanga wa kiroho bali pia kanuni zisizopitiwa na wakati zinazoelekeza kwenye mwenendo wa kimaadili, uadilifu, huruma, na kujitahidi kwa kuendelea kwa ubora katika nyanja zote za maisha, Fadillah amesema.
Amewataka viongozi kupata msukumo kutokana na mafundisho ya Qur'ani ili kuongoza matendo na maamuzi yao.
Fadillah amesema ilie fikra ya Malaysia ya MADANI, iliyoletwa na serikali, inazingatia kanuni za Qur'ani na Sunnah. "Kwa kuunganisha mafundisho haya ya Qur'ani katika utendaji wa usimamizi wa shirika, viongozi wanaweza kukuza mazingira ambayo yanakuza maadili, kufanya maamuzi shirikishi, uvumbuzi, na ushirikishwaji wa jamii," amesema.
Amesisitiza kuwa mwenendo wa kimaadili, mafundisho ya msingi ya Qur'ani, ni pamoja na kudumisha uadilifu, uaminifu na uwazi katika utawala. “Uadilifu ni miongoni mwa kanuni kuu za Qur’an, ambayo inatuelekeza ‘kusimama imara kwa ajili ya uadilifu, kama mashahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, hata ikiwa ni dhidi ya nafsi zenu au wazazi na jamaa (4:135)’” Fadillah alibainisha.
Fadillah alitoa wito wa kuunganishwa kwa mafundisho ya Qur'ani katika mfumo wa utawala, sera, na maisha ya kibinafsi. "Kwa kufanya hivyo, tunaweza kuzingatia maadili adhimu yaliyowekwa katika imani yetu na kutimiza wajibu wetu wa kuliongoza taifa letu kuelekea mustakbali mwema na wenye mafanikio zaidi," alihitimisha.

3490220

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu malaysia
captcha