IQNA

Afisa wa Malaysia: Qur'ani Mwongozo kwa Kila Hatua Maishani

16:46 - March 19, 2025
Habari ID: 3480402
IQNA – Waziri mmoja wa Malaysia ameitaja Qur'ani kama nuru inayoongoza na dira kwa kila hatua maishani.

Katika taarifa yake Jumanne (Machi 18), katika hafla inayojulikana kama Nuzul Qur'ani, Waziri katika Idara ya Waziri Mkuu, Dk. Mohamad Na’im Mokhtar, alisema kuwa Wamalaysia wote wanapaswa kutumia fursa ya Ramadhani hii kujifunza kuhusu Qur'ani.

"Qur'ani ni nuru inayoongoza, tiba kwa moyo, na dira kwa kila hatua maishani," alisema Mohd Na’im.

"Katika usiku huu uliobarikiwa, tutafakari maana halisi ya Nuzul Qur'ani kwa kujikurubisha zaidi na maneno ya Allah, kuimarisha ufahamu wetu, na kuyatendea kazi mafundisho yake katika maisha yetu ya kila siku," aliongeza. 

"Kama waja wa Allah, tunapaswa kujitahidi kuifanya Qur'ani kuwa rafiki mwaminifu, chanzo cha nguvu, na mwongozo katika kila uamuzi tunaochukua. Tunamuomba usiku huu maalum ulete baraka kwa wote na kuimarisha imani na ibada yetu kwake," alisema.

"Naomba Wamalaysia wote kutumia fursa hii katika mwezi huu wa rehema kwa kuongeza usomaji wa Qur'ani, kutafakari aya zake, na kukumbatia maadili yake matukufu," aliongeza Dr. Na'im. 

Nuzul Qur'ani katika kalenda ya Kiislamu inaadhimisha usiku ambao aya ya kwanza ya Qur'ani inasadikika na Waislamu fulani kuwa iliteremshwa kwa Mtume Muhammad (SAW) tarehe 17 ya Ramadhani, katika Pango la Hira, Mecca.

3492436

Habari zinazohusiana
Kishikizo: malaysia qurani tukufu
captcha