IQNA

22:11 - December 06, 2020
Habari ID: 3473430
TEHRAN (IQNA) – Klipu ya qiraa ya Qur'ani Tukufu ya mtoto Mwafrika ambayo imesambazwa katika mitandao ya kijamii imewavutia wengi nchini Iran na kote duniani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, qiraa ya Qur'ani Tukufu yenye mvuto ya mtoto Mwafrika ambaye anaaminika kuwa ni mkaazi wa Zanzibar nchini Tanzania, imewavutia wanaharakati wengi wa Qur'ani katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Miongoni mwa waliovutiwa na qiraa hiyo ni Ustadh Abul Qassimi ambaye ni mwalimu na qarii wa kimataifa wa Qur'ani na pia Bi. Samia Hajali ambaye ni mkurugenzi wa Darul Qur'an Imam Ali AS miongoni mwa wengine wengi.

Wengi ya waliosikilizaji qiraa hiyo wametaka kumfahamu mtoto huyo ili kipawa chake kiweze kuimarishwa zaidi.

Hii hapa chini klipu hiyo

کد ویدیو

3939262

Kishikizo: qiraa ، mtoto ، mtanzania ، qurani tukufu
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: