IQNA

Mtanzania miongoni mwa washindi Mashindano ya Qur'ani kwa Wanawake Dubai

9:49 - November 26, 2017
Habari ID: 3471281
TEHRAN (IQNA)-Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Dubai kwa wanawake yamemalizika kwa kutunukiwa zawadi washindi.
Mtanzania miongoni mwa washindi Mashindano ya Qur'ani kwa Wanawake DubaiMashindano hayo ambayo ni maarufu kama Mashindano ya Qur’ani ya Sheikha Fatima Bint Mubarak yalifanyikia baina ya tarehe 12-24 Novemba ambapo kulikuwa na washiriki 76 walioshindana katika ukumbi wa Jumuiya ya Sayansi na Utamaduni katika eneo la Mamzar mjini Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu.

Mshindi wa mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu alikuwa ni Hadil Khalid wa Palestina ambaye alipata zawadi ya Dirhamu 250,000. Ramla Hassan wa Finland alishika nafasi ya pili na kupata zawadi Dirhamu 200,000, huku Israa Husam wa Bahrain na Noura Muhammad Ahmad wa Marekani wakishika nafasi ya tatu kwa pamoja na hivyo kila moja wao akipata zawadi ya Dihramu 150,000.

Washindi wa kitengo cha 'usomaji maridadi zaidi' walikuwa Salma Mohammad wa Morocco huku nafasi ya pili ikishikwa na Zakia Juma Ramadhan wa Tanzania na Reem Monther wa Jordan.

3464506

captcha