IQNA

20:45 - December 18, 2020
Habari ID: 3473469
TEHRAN (IQNA)- Qiraa ya Qur’ani Tukufu ya qarii wa Misri marhum Sheikh Ahmed Mohammed Amer hivi karibuni imerushwa hewani katika televisheni ya Qur’ani ya Iran.

Katika qiraa hiyo, Sheikh Amer anasema aya za Surah Maryam katika Qur’ani Tukufu.

Sheikh Amer alizaliwa mwaka 1927 katika mji wa Faqus katika jimbo la Ash Sharqiya nchini Misri ambapo alijifunza Qur’ani akiwa na umri mdogo. Aidha alipata mafunzo ya qiraa ya Qur’ani Tukufu na kubobea zaidi katika taaluma hiyo kadiri umri ulivyozidi kuongezeka.

Sheikh Amer alijiunga na Radio ya Misri kama qarii wa Qur’ani akiwa na umri wa miaka 36.

Sheikh Amer alitembelea nchi mbali mbali duniani kama vile Palestina, Brazil, Uingereza, Marekani, Ufaransa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kushiriki katika vikao vya qiraa ya Qur’ani. Sheikh Amer kwa mara kadhaa alikuwa katika jopo la majaji wa mashindano ya kimatiafa ya Qur’ani nchini Iran.

Sheikh Ahmed Amer, aliaga dunia mwezi Februari mwaka 2016 akiwa na umri wa miaka 89.

3941113

Kishikizo: qiraa ، qurani tukufu ، misri ، AMER
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: