IQNA

Hamas yafanya mazungumzo na nchi kadhaa kuhusu uchaguzi Palestina

12:39 - January 10, 2021
Habari ID: 3473544
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi mwandamizi Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amewaomba baadhi ya viongozi wa nchi ikiwemo Iran kuunga mkono juhudi zilizofanyika kwa ajili ya kuimaisha umoja na mshikamano wa kitaifa wa Palestina.

Ismail Hania, Mkuu wa Idara ya Siasa ya Hamas ametuma barua kwa Umoja wa Mataifa na pia kwa viongozi wa Iran, Jordan, Uswisi na Afrika Kusini akibainisha misimamo ya harakati hiyo kuhusu juhudi zilizofanyika kwa ajili ya kuimarisha umoja wa kitaifa huko Palestina na suala la kuitishwa uchaguzi mkuu.

Wiki iliyopita Haniyah pia alitilia mkazo azma ya Hamas ya kufanikisha mchakato wa kuimarisha mapatano ya kitaifa ya Palestina na kuwepo mwafaka baina ya vyama na makundi yote kwa ajili kukabiliana na utawala ghasibu na kukomboa Quds tukufu. 

Duru zinadokeza kuwa siku chache zikazo Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina atatoa dikri ya kuitishwa uchaguzi mkuu na kwamba uchaguzi huo umepangwa kufanyika katikati ya mwezi Mei mwaka huu. 

Itakumbukwa kuwa mwezi Disemba mwaka uliopita makatibu wakuu wa vyama na makundi ya Palestina walikutana mjini Istanbul, Uturuku na kuafikiana juu ya suala la kuitishwa chaguzi za Bunge na Rais haraka iwezekanavyo.    

3946678

captcha