IQNA

Harakati za Palestina zaafiki tangazo la uchaguzi mkuu

11:15 - January 16, 2021
Habari ID: 3473561
TEHRAN (IQNA) - Harakati za kupigania ukombozi wa Palestina za Fat'h na Hamas zimeunga mkono tangazo la Mamlaka ya Ndani ya Palestina kuhusu kufanyika uchaguzi wa bunge la rais baadaye mwaka huu.

 

Katika taarifa Ijumaa usiku, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imesisitiza kuwa, tangazo hilo ni mafanikio kwa watu wa Palestina ambao wana haki ya kuwachagua viongozi wao.

Harakati ya Hamas imesisitiza kuwa katika miezi ya hivi karibuni imekuwa ikijitahidi kuondoa vizingiti vyote katika kufikia mapatano ya kufanya uchaguzi. 

Harakati ya Fat'h nayo pia imeunga mkono tangazo ya kufanyika uchaguzi mkuu wa Palestina na kusema uchaguzi huo utakuwa ni dhihirisho la irada ya watu wa Palestina.

Msemaji wa Fat'h Osama al-Qawasemi amesema Wapalestina wanapita katika kipindi cha kihisotoria na hivyo hatua muhimu itakayofuata ni mazungumzo ya kitaifa kuhusu masuala yote.

Siku ya Ijumaa  Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina, Mahmoud Abbas, alitangaza tarehe za kufanyika uchaguzi wa Palestina baada ya mkutano na Hana Nasser, Mkuu wa Kamati ya Uchaguzi Palestina.

Kwa mujibu wa tangazo uchaguzi wa bunge utafanyika Mei 22 na utafuatiwa na uchaguzi wa rais mnamo Julai 31. Baadi ya hapo, mnamo Agosti 31 kutafanyika uchaguzi wa Baraza la Kitaifa la Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) ambayo huwakilisha Palestina kimataifa. 

3473709

captcha