IQNA

20:46 - January 21, 2021
News ID: 3473577
TEHRAN (IQNA)- Ghasia zimeibuka maeneo kadhaa Marekani baada ya Joe Biden kuapishwa kama rais wa 46 wa Marekani siku ya Jumatano.

Taarifa zinasama waandamnaji hao ambao walikuwa ni wafuasi wa  kundi la ANFITA wameteketeza moto bendera za Marekani.

Baada ya kumalizika uchaguzi uliogubikwa na utata mwingi, hatimaye Joe Biden aliapishwa kuwa rais wa 46 wa Marekani

Katika hutuba yake ya kwanza akiwa Rais wa Marekani, Biden amsisistiza juu ya masuala muhimu ambayo ni pamoja na 'demokrasia ya Marekani' na 'umoja wa kitaifa' miongoni mwa Wamarekani. Amesema matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika hivi karibuni ni ushindi kwa demokrasia na kuitaka mirengo yote ya kisiasa ya nchi hiyo kuweka kando hitilafu zao.

Pamoja na hayo lakini matukio ya miezi kadhaa iliyopita yanathibitisha wazi kwamba kudhoofika misingi ya demokrasia na mapengo ambayo yamedhihiri kati ya matabaka mbalimbali ya Wamarekani ni makubwa kiasia kwamba hayawezi kuzibwa kwa maneno matupu ya rais mpya wa nchi hiyo. Hata hivyo ni wazi kuwa viongozi wa ngazi za juu wa serikali na wanasiasa mashuhuri wa Marekani, bila shaka ukiachilia Donald Trump rais aliyeondoka madarakani na wanasiasa wengine wa karibu yake, wanapasa kusisitiza juu ya umuhimu wa kulindwa umoja wa kitaifa na kuimarishwa misingi ya demokrasia nchini.

Pamoja na hayo, hotuba zilizotolewa katika nukta mbili tofauti za mji mkuu wa Marekani Washington, yaani moja katika ikulu ya White House wakati wa kuondoka madarakani Trump, na katika Congress, wakati wa kuingia madarakani Joe Biden, zinathibitisha wazi ni kwa kiwango gani jamii ya Marekani imegawanyika. Trump ameondoka madarakani bila kuhudhuria sherehe za kuapishwa Biden naye Biden katika hotuba ya ufunguzi wa urais wake  hakuashiria hata kwa neno moja nafasi ya Trump katika utawala wa nchi hiyo. Hii ni katika hali ambayo askari walinda-usalama zaidi ya 25,000 waliwekwa sehemu maalumu kulinda usalama wa sherehe hiyo ya kuapishwa Rais Biden na hivyo kuzidi hata idadi ya wageni waalikwa.

هرج و مرج و آشوبگری در پورتلند بعد از مراسم تحلیف جو بایدن
 
3949071

Tags: biden ، marekani ، trump ، ghasia
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: