IQNA

Harakati ya Ansarullah ya Yemen yaonya italenga kwa mabomu viwanja vya ndege Saudia

15:47 - February 11, 2021
Habari ID: 3473642
THERAN (IQNA)- Mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Asarullah ya Yemen amesisitiza kuwa, Utawala wa Aal Saud unatumia viwanja vya ndege vya Saudia kutekeleza mashambulizi dhidi ya Yemen na kuyatahadharisha mashirika ya ndege kutotumia viwanja hivyo.

Muhammad  al Bakhiti amesema kuwa, anayanasihi mashirika ya ndege kutotumia viwanja vya ndege vya Saudi Arabia kwa sababu viwanja hivyo vinatumika kuendeshea mashambulizi dhidi ya Yemen na kuizingira nchi hiyo. 

Al Bakhiti ametahadharisha kuwa, viwanja hivyo vya ndege ni maeneo halali na ya kisheria ya kulengwa na mashambulizi ya majeshi ya Yemen. 

Mwakilishu wa ngazi ya juu wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza pia juu ya kuilinda nchi yake na kukabiliana na nchi vamizi na kueleza kuwa, Yemen inataka kusimamishwa vita dhidi yake na kurejeshwa amani nchini lakini haiafiki mapatano ya upande mmoja. 

Jana Jumatano duru za habari zilitangaza kuwa, ndege za kivita za Saudia Arabia zimeshambuliwa katika uwanja wa ndege wa Abha na ndege nne za Yemen zisizo na rubani (droni).  

Wakati huo huo Msemaji wa Jeshi la Yemen Yahya Saree ametangaza kuwa Wasaudia walikuwa wakitumia uwanja huo wa ndege kuwashalia wananchi wa Yemen na ndio maana umeshambuliwa. 

Ikumbukwe kuwa mnamo mwezi Machi 2015 Saudi Arabia, ikiungwa mkono na  Marekani, utawala haramu wa Israel, Umoja wa Falme za Kiarabu  na nchi zingine kadhaa iliivamia kijeshi Yemen na kuiwekea mzingiro wa kila upande.

Utawala dhalimu wa Saudia ulianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen kwa lengo la kuiondoa madarakani Harakati ya Ansarullah na kumrejesha madarakani kibaraka wake, Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kukimbilia Riyadh. Hata hivyo hadi sasa Saudia na washirika wake wameshindwa kufikia malengo yao kutokana na kusimama kidete wananchi wa Yemen wakiongozwa na Harakati ya Ansarullah. Harakati hiyo imekuwa ikitekeleza mashambulizi ya kulipiza kisasi ndani ya ardhi ya Saudi Arabia ambapo imeleng mara kadhaa vituo vya kusafisha mafuta na pia viwanja vya ndege vinavyotumiwa na jeshi vamizi la utawala huo wa kifalme.

Hivi karibuni, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) lilisema kati ya Januari na Juni 2021, asilimia 54 ya Wayemen, yaani watu milioni 16.2, watakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na vita vya Saudia dhidi ya nchi hiyo..

Aidha mwezi Disemba mwaka jana,  Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) ilitangaza kuwa vita vya Saudi Arabia dhidi ya Yemen vimepelekea zaidi ya watu 233,000 kupoteza maisha katika kipindi cha miaka sita iliyopita.

3473948/

captcha