IQNA

Maulamaa wa Yemen walaani hatua ya Marekani dhidi ya Ansarullah

20:13 - January 12, 2021
Habari ID: 3473550
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya ya Maulamaa wa Yemen imetoa taarifa na kulaani vikali hatua ya Marekani kutangaza kuwa Harakati ya Mamapmbano ya Kiislamu ya Ansarullah nchini Yemen ni kundi la 'kigaidi'.

Katika taarifa, jumuiya hiyo imeutaja uamuzi huo kuwa wa kisiasa na ambao utakuwa na matokeo mabaya kwa rais wa Marekani na utawala wake.

Aidha wanazuoni hao wa Kiislamu wamesisitiza kuwa uamuzi kama huo utaimarisha zaidi azma imar aya watu wa Yemen katika kusimama kidete kukabiliana na njama za Marekani za kutaka kuitawaka nchi yao. Halikadhalika wamesema uamuzi huo wa Marekani utawafanya wananchi wa Yemen kuunga mkono harakati ya Ansarullah katika mapambano yake dhidi ya wavamizi wanaoongozwa na Saudia.

Siku ya Jumapili Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alitangaza mpango wa kuitangaza Harakati ya Ansarullah kuwa ni 'kundi la kigaidi' kwa mujibu wa sheria za Marekani.

Akijibu tuhuma hizo, msemaji wa Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen Zaifullah al Shami  amesema kuwa Marekani imetumia njia zote kwa ajili ya kuliangamiza taifa la Yemen na nchi hiyo ndio kinara wa ugaidi duniani.

Al Shami amesema kitendo cha Marekani cha kuitaja harakati ya Ansarullah kuwa ni kundi la kigaidi kumeweka wazi kilele cha jinai zilizotekelezwa na nchi hiyo dhidi ya watu wa Yemen na kuongeza kuwa, kitendo hicho cha Marekani si tu hakiathiri mwelekeo wa kijeshi au kijamii wa vikosi vya Yemen bali kinazidisha nguvu na azma ya vikosi hivyo. 

Ikumbukwe kuwa mnamo mwezi Machi 2015 Saudi Arabia, ikiungwa mkono na  Marekani, utawala haramu wa Israel, Umoja wa Falme za Kiarabu  na nchi zingine kadhaa iliivamia kijeshi Yemen na kuiwekea mzingiro wa kila upande.

Utawala dhalimu wa Saudia ulianzisha mashambulizi dhidi ya Yemen mwishoni kwa lengo la kuiondoa madarakani Harakati ya Ansarullah na kumrejesha madarakani kibaraka wake, Abdrabbuh Mansour Hadi, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kukimbilia Riyadh. Hata hivyo hadi sasa Saudia na washirika wake wameshindwa kufikia malengo yao kutokana na kusimama kidete wananchi wa Yemen.

3947273

captcha