IQNA

Kiongozi wa Ansarullah
17:18 - February 20, 2021
Habari ID: 3473667
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza kuwa watu wa nchi hiyo hawatawekwa chini ya mamlaka ya Saudi Arabia, Imarati, Marekani au utawala wa Kizayuni wa Israel.

Sayyid Abdulmalik Badruddin al Houthi ameyasema hayo jana kwa mnasaba wa Ijumaa ya mwanzo ya mwezi wa Rajab na akasisitiza: "Sisi hatutaki kuwa chini ya mamlaka ya Saudia, Imarati, Marekani, Israel au nchi nyingine yoyote ile. Sisi tumekomboka; na utambulisho wetu wa kiimani unatutaka tufanye juhudi ili tuhakikishe tunajitawala."

Kiongozi wa Ansarullah amebainisha kuwa, serikali ya uokovu wa kitaifa ya nchi hiyo ina lengo moja, ambalo ni kukabiliana na wavamizi na ujikwezaji wa maajinabi.

Sayyid Abdulmalik al Houthi ametahadharisha pia juu ya kujitokeza harakati ya ukufurishaji ndani ya Yemen na akasema, harakati hiyo iko mbali na watu wa Yemen na wala haikubaliani na asili ya utambulisho na imani ya watu wa wa nchi hiyo.

Kila mwaka katika Ijumaa ya mwanzo ya mwezi wa Rajab, Wayemeni huwa wanafanya sherehe maalumu. Ilikuwa ni katika siku hiyo ambapo watu wa ardhi hiyo walipoukubali na kuupokea wito wa mjumbe wa Bwana Mtume Muhammad SAW, Imam Ali AS wa kusilimu na wakasali Sala ya kwanza ya Ijumaa iliyoongozwa na Imam Ali AS.

3474025/

Kishikizo: Ansarullah ، yemen
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: