IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Mapinduzi ya Kiislamu Iran yakifuata mafundisho ya kubaathiwa Mtume SAW yamesimama kidete mbele ya dhulma

19:57 - March 11, 2021
Habari ID: 3473726
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, sikukuu kubwa ya Mab’ath na kumbukumbu ya kubaathiwa na kupewa Utume Mtume Muhammad SAW ni ya wapigania uadilifu kote ulimwenguni.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo mjini Tehran wakati akihutubu kwa njia ya televisheni kwa mnasaba wa sikukuu ya Mab’ath na kubaathiwa Mtume SAW na kubainisha kwamba, katika siku kama ya leo, moyo wa Mtume uligeuka na kuwa mahala penye kuweke kito cha thamani kubwa ambacho ni amana ya Mwenyezi yaani Wahyi na Ufunuo.

Ayatullah Khamenei ameashiria chuki za madhalimu wa dunia dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kwamba, hii leo pia mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu unaandamwa na mawimbi ya kila aina ya hujuma na njama, na hiyo ni kwa sababu mfumo huu umeweza kuanzisha utawala wa sheria za Mwenyezi Mungu na kuwapatia wananchi wa taifa hili utambulisho wa kidini na Kiislamu.

3959040

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu sambamba na kueleza kuwa, taifa hili likifuata mafundisho ya kubaathiwa Mtume SAW limesimama kidete mbele ya dhulma, ubeberu na uistikbari na daima limekuwa pamoja na wanyonge na wanaodhulumiwa ameongeza kuwa,  baada ya kuundwa mfumo wa Kiislamu hapa nchini kulianza kushuhudiwa matukio yale yale yaliwakumba Mitume wa Allah ambapo mabeberu na watu makatili wamesimama katika safu moja dhidi ya taifa la Iran. 

Ayatullah Khamenei amesema pia kuwa, kupotosha ukweli wa mambo ni moja ya mbinu za adui katika vita laini ambapo sanjari na kuashiria mifano ya uwongo wa wazi amesema kuwa, wananchi madhulumu wa Yemen kwa miaka sita sasa wamekuwa wakishambuliwa kwa mabomu na kukabiliwa na mzingiro wa kiuchumi, chakula na dawa kufuatia hujuma na vita vilivyoazishwa na utawala wenye roho mbaya na wa kidhalimu wa Saudi Arabia kwa himaya ya Marekani, na hakuna sauti yoyote ile ya kulalamikia hilo inayosikika katika asasi za kimataifa na katika madola ya Magharibi yanayodai kuwa ni watetezi wa haki za binadamu.

captcha