IQNA

11:41 - March 26, 2021
News ID: 3473763
TEHRAN (IQNA) – Hivi sasa katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mataifa kadhaa ya karibu wananchi wanaadhimisha kuwadia mwaka mpya wa Hijria Shamsiya.

Mwaka huu huanza sambamba na kuwadia msimu wa machipuo ya mimea na hivyo huambatana na mzunguko wa mazingira asilia.

Kwa mnasaba huu tunawaleteeni qiraa ifuatayo ya qarii wa Misri  Ustadh Faruq Zaif  akisoma aya ya 99 ya Suurat An'aam katika Qur'ani Tukufu inayohusu machipuo, maumbile na mazingira asilia. Aya hiyo inasema: Na Yeye ndiye anaye teremsha maji kutoka mbinguni; na kwayo tunatoa mimea ya kila kitu. Kutokana na baadhi yao tukatoa mimea ya majani, tukatoa ndani yake punje zilizo pandana; na kutokana na mitende yakatoka kwenye makole yake mashada yaliyo inama; na bustani za mizabibu na mizaituni, na makomamanga, yaliyo fanana na yasiyo fanana. Angalieni matunda yake yanapo zaa na yakawiva. Hakika katika hayo pana Ishara kwa watu wanao amini.

Tarehe Mosi Farvardin inayosadifiana na Machi 20 au 21 huwa siku ya kwanza ya mwaka wa Hijria Shamsiya. Siku hii ambayo ni mwanzo wa msimu maridadi wa machipuo hapa nchini ni maarufu kwa jina la Sikukuu ya Nowruz au Nairuzi kwa lugha ya Kiswahili. Nowruz au Nairuzi kwa lugha ya Kiswahili ni moja kati ya sherehe za kale zaidi duniani na ilianza kusherehekewa zaidi ya miaka 3000 iliyopita. Mbali na Iran nchi ambazo husherehekea Nowruz ni pamoja na Afghanistan, Jamhuri ya Azerbaijan, Albania, Kyrgyzstan, Turkmenistan, Macedonia, India, Uturuki, Jamhuri ya Tatarstan nchini Russia, Sudan na Zanzibar nchini Tanzania. Mwaka 2010 Umoja wa Mataifa ulitangaza rasmi tarehe Mosi Farvardin yaani 21 Machi kila mwaka kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Nowruz. Umoja wa Mataifa umeitambua Siku ya Nowruz kama siku kuu ya kale ambayo huadhimishwa wakati wa kuwadia msimu wa machipuo na kuhuishwa tena mazingira.

3960174

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: