IQNA

Mwezi wa Ramadhani

Ramadhani 2024: Ni nchi gani zilizoanza Ramadhani siku ya Jumatatu?

17:17 - March 11, 2024
Habari ID: 3478486
IQNA - Nchi kadhaa zimetangaza Jumatatu, Machi 11, kuwa siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu, huku zingine zingine zikitangaza kuwa kuwa ni keshi Jumanne.

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, ambao sawa na miezi mingine ya hutegemea kuandama mwezi,  hupelekea kuwepo mitazamo tofauti ya kifiqhi kuhusu namna ya kubaini huanza mwezi huu mtukufu.

Saudi Arabia, pamoja na mataifa kadhaa ya Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi  na nchi kama Iraq, Syria, na Misri, zilianza kufunga siku ya Jumatatu.

Kinyume chake, baadhi ya mataifa katika eneo la Asia-Pasifiki, ikiwa ni pamoja na Australia, Brunei, Indonesia, Malaysia, na Singapore, pamoja na Oman na Jordan, yataanza Jumanne baada ya wataalamu kuwa mwezi mwandamo haukuonekana jana jioni.

Jamhuri ya Kiisalmu ya Iran pia imetangaza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani utaanza siku ya Jumanne huku ofisi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatollah Seyyed Ali Khamenei ikithibitisha tarehe hiyo baada ya timu za "Istihlal" (kutafuta mwezi mwandamo) kubaini kuwa mwezi haukuonekana siku ya Jumapili.

 Mwezi wa Ramadhani (ambao huenda ikaanza Machi 12 mwaka huu) ni mwezi wa tisa wa kalenda ya Kiislamu. Qur'ani Tukufu iliteremshwa kwenye moyo wa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) katika mwezi huu. Mwezi huu mtukufu ni kipindi cha kukithirisha sala, saumu, utoaji wa sadaka na uwajibikaji kwa Waislamu duniani kote.

Wakati wa Ramadhani, Waislamu hufunga (kujiepusha na vyakula na vinywaji na yote yaliyokatazwa) kuanzia wakati wa kabla ya Sala ya Afajiri hadi Magharibi.

Mwaka huu vita vya Israel dhidi ya Gaza vimeugubika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo Wapalestina Waislamu wameathiriwa na ghasia na kufurushwa makwao.

Hali katika Gaza bado ni mbaya, ambao mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala katili wa Israel yamepelekea kuuawa Wapalestina takriban watu 31,000, wengi wakiwa ni wanawake na watoto na zaidi ya 72,000 wakijeruhiwa katika mashambulizi yaliyoanza Oktoba 7 huku kukiwa na wasiwasi wa njaa kubwa.

Mvutano unaweza pia kuongezeka kutokana na vikwazo vya kuswali kwa Waislamu katika Msikiti wa Al-Aqswa katika eneo la Quds (Jerusalem) linalokaliwa kwa mabavu.

3487514

Kishikizo: ramadhani nchi
captcha