IQNA

Kadhia ya Palestina

Ansarullah ya Yemen: Waislamu waifanye Ramadhani kuwa Mwezi wa kuunga mkono Gaza

16:02 - March 07, 2024
Habari ID: 3478464
IQNA - Msemaji wa Harakati ya Ansarullah inayotawala Yemen amesisitiza kwamba jambo muhimu zaidi kwa Waislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ni uungaji mkono kwa Wapalestina wanaoteseka huko Gaza.

Katika chapisho kwenye akaunti yake ya X siku ya Jumatano, Muhammad Abdul Salam alisema kuunga mkono Gaza katika Mwezi wa Ramadhani jambo lenye umuhimu mkubwa sana.

Alitoa wito kwa Umma wa Kiislamu kuufanya mwezi mtukufu kuwa wakati wa kuhamasisha uungaji mkono na usaidizi kwa Wapalestina wa Ukanda wa Gaza ambao wanakabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendesha na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa himaya ya Marekani.

Kwa zaidi ya siku 150, watu wa Gaza wamestahimili kile ambacho milima haikuweza kustahimili, alisema.

Abdul Salam ameongeza kuwa mataifa na serikali za Kiislamu zinapaswa kutambua wajibu wao kuhusu Gaza na kufanya kila wawezalo ili kukomesha mashambulizi ya kinyama ya adui katika eneo hilo la Palestina.

Yemen inasisitiza msimamo wake madhubuti wa kuunga mkono Gaza na inakaribisha miito ya harakati za Wapalestina za kutaka kuimarishwa uungaji mkono kwa watu wa Gaza katika mwezi wa Ramadhani, alisema.

Msemaji huyo aidha amesema kila tone la damu la Wapalestina linalomwagika huko Gaza ni fedheha kwa Marekani inayounga mkono utawala dhalimu wa Israel.

Uimara wa watu wa Gaza katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita umethibitisha kwamba watakuwa washindi kwa neema ya Mwenyezi Mungu, aliendelea kusema.

Israel ilianzisha mauaji ya kimbarii katika Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 7, na hadi sasa utawala huo dhalimu umeuawa zaidi ya Wapalestina 31,000, wengi wakiwa ni wanawake na watoto na kujeruhi wengine zaidi ya 72,000 huku kukiwa na uharibifu mkubwa na uhaba wa mahitaji ya dharura.

Israel pia imeweka vizuizi vya kulemaza katika Ukanda wa Gaza, na kuwaacha wakazi wake, hasa wakaazi wa kaskazini mwa Gaza, kwenye hatihati ya njaa.

Vita vya Israel vimesukuma 85% ya wakazi wa Gaza kuhama makazi yao huku kukiwa na uhaba mkubwa wa chakula, maji safi na dawa, wakati 60% ya miundombinu ya eneo hilo imeharibiwa, kulingana na UN.

Israel inashutumiwa kwa mauaji ya kimbari katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki. Katika miezi ya hivi karibuni, vikosi vya Yemen vimekuwa vikiendesha mashambulizi dhidi ya meli za Israel au zile zinazoelekea katika bandari za zinazokaliwa kwa mabavu na Israel. Operesheni hizo zimeelezewa kama jibu kwa vita vya mauaji ya halaiki ya Israeli na kuzingirwa kwa Gaza.

 4203944

Habari zinazohusiana
captcha