IQNA

Kiongozi Muadhamu katika ujumbe kwa mnasaba wa Siku ya Jeshi nchini Iran
19:31 - April 17, 2021
News ID: 3473824
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe maalumu kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Jeshi nchini Iran.

Aidha amesisitiza kuwa, jeshi liko imara katika medani kwa ajili ya kutekeleza vizuri majukumu yake. Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo ikiwa ni sehemu ya kuienzi Siku ya Jeshi na hamasa kubwa ya jeshi la nchi kavu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akimsisitizia Meja Jenerali Sayyid Abdul Rahim Mousavi, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu kwamba jeshi liko imara katika medani kwa ajili ya kutekeleza vilivyo majukumu yake, hivyo hakikisheni utayari huo uko kwa kiwango cha juu kinachowezekana kwa ajili ya kutekeleza majukumu kwa namna bora kabisa.

Amirijeshi Mkuu wa majeshi yote ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia amewapongeza wafanyakazi, na familia za maafisa za vikosi vya ulinzi vya Iran.

3965150

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: