IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya watu wenye Ulemavu yakamilika Saudi Arabia

17:18 - October 22, 2022
Habari ID: 3475972
TEHRAN (IQNA) – Msikiti mmoja katika mkoa wa Ha'il nchini Saudi Arabia ulikuwa mwenyeji wa hafla ya kufunga mashindano ya Qur'ani kwa watu wenye ulemavu.

Maafisa kadhaa wa eneo hilo pamoja na wale kutoka wizara ya masuala ya Kiislamu, Dawah, na Mwongozo walihudhuria hafla hiyo katika msikiti mkuu wa Rajihi.

Mashindano hayo yaliandaliwa na Jumuiya ya Walemavu katika eneo la Ha'il kwa msaada kutoka kwa Wakfu wa Al-Ajimi, mkuu wa bodi ya wakurugenzi wa jumuiya hiyo alisema katika hotuba yake.

Ameongeza kuwa mashindano hayo yalilenga kubainisha vipaji katika kuhifadhi na kusoma Qur'ani miongoni mwa walemavu wa eneo hilo.

Washindi wa shindano hilo pamoja na wajumbe wa jopo la majaji walitunukiwa katika hafla hiyo.

Maafisa wa wizara ya masuala ya Kiislamu, Dawah, na mwongozo pia waliwashukuru wale walioshikilia na kuunga mkono tukio hilo la Qur'ani.

4093401

captcha