IQNA

Sayyid Hassan Khomeini

Mapinduzi ya Kiislamu yakiongozwa na Imam Khomeini (MA) yaliirekebisha jamii

11:18 - June 04, 2021
Habari ID: 3473977
TEHRAN (IQNA)- Ujumbe muhimu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ulikuwa ni kutoa wito kwa dunia ya sasa irejee katika umaanawi na maadili mema.

Hayo yamesemwa na mjukuu wa Imam Khomeini-Mwenyezi Mungu Amrehemu-, Hujjatul Islam Sayyed Hassan Khomeini  Alhamisi mjini Tehran alipohutubu katika Kongamano la Kimataifa la 'Imam Khomeini na Ulimwengu wa Kisasa". Kongamano hilo limefanyika  kwa munasaba wa kukumbuka mwaka wa 32 wa kuaga dunia Imam Khomeini MA, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Amesisitiza kuwa,  ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu miaka 43 iliyopita haukuwa na taathira katika mipaka ya Iran tu bali ujumbe wake ulifika katika nchi za Kiislamu na zisizo za Kiislamu.

Sayyed Hassan Khomeini ameongeza kuwa Mapinduzi ya Kiislamu yaliirekebisha jamii na kulea wanasayansi katika vijiji sambamba na kulea kizazi kipya ambacho kimeinukia na mafunzo ya Imam Khomeini MA.

Halikadhlika amesema Imam Khomeini aliweza kulifanya taifa la Iran lifungamane na dini na kuongeza kuwa, 'moja ya turathi muhimu za Imam Khomeini ni Jamhuri ya Kiislamu'. Aidha amesema ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yakiongozwa na Imam Khomeini, uliashiria kuangamia daima mfumo wa ufalme nchini Iran.

3975309/

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :