IQNA

Mapinduzi ya Kiislamu

Rais Ebrahim Raisi: Maisha yote ya Imam Khomeini (MA) yalikuwa ni ya kupinga uistikbari

21:23 - January 31, 2024
Habari ID: 3478281
IQNA-Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kadhia kuu nambari moja ya Ulimwengu wa Kiislamu ni Palestina na ukombozi wa Quds Tukufu, Kibla cha Kwanza cha Waislamu, kutoka kwenye makucha ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Rais Ebrahim Raisi amesema hao leo Jumatano wakati wa kukaribia kuingia maadhimisho ya Alfajiri Kumi na mwaka wa 45 wa ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran. 

Amesema hayo wakati yeye na Baraza lake la Mawaziri walipokwenda kwenye Haram ya Imam Khomeini, mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ili kutangaza upya uaminifu wao kwa malengo matakatifu ya Mapinduzi ya Kiislamu na kuongeza kuwa, Imam Khomeini MA alisema kuwa, dola ghasibu na pandikizi la Kizayuni litaangamia tu na wakati leo tunapoangalia uhalisia wa mambo duniani tunaona wazi kuwa bishara hiyo imekaribia sana kutokea.

Amesema, maisha yote ya Imam Khomeini yalikuwa ni ya kupinga uistikbari na kuongeza kwamba, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran bado yako imara katika msimamo wake wa kupinga ubeberu na fikra hiyo imepata nguvu sana leo hii kote ulimwenguni kiasi kwamba katika kila kona ya dunia hivi sasa kunashuhudiwa hisia kali za kupinga uistikbari na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel. 

Rais Raisi pia amesema, taifa kubwa la Iran limefanya jitihada za kufelisha njama za adui katika nyuga tofauti hasa kutokana na kutambulisha kwake msingi wa misimamo ya wastani na vielelezo vyake duniani na kutoa bishara ya kudhihiri ustaarabu mpya ulimwenguni. 

Amegusia pia kukaribia uchaguzi wa Majlis ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) na wa Baraza la Wanavyuoni Wataalamu na kubainisha kwamba, ni jambo muhimu sana kuzingatia mfumo wa jamhuri uliosimama juu ya msingi wa kura za na chaguo la wananchi.

4197048

Habari zinazohusiana
captcha