IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya wanafunzi yafanyika Uganda

14:01 - June 17, 2021
Habari ID: 3474015
TEHRAN (IQNA)- Mashindano ya Kuhifadhi na Kusoma Qur'ani ya wanafunzi yamefanyika hivi karibuni nchini Uganda.

Mashindano hayo yameandaliwa kwa pamoja na Shirika la Televisheni ya Kitaifa UBC na Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini Uganda ambapo wanafunzi 50 walishiriki.

Washindi katika kategoria hizo mbili walitunukiwa zawadi katika sherehe iliyohudhuriwa na maafisa wa UBC na wasomaji Qur'ani mashuhuri nchini humo.

Akizungumza katika hafla hiyo Faridah Ali Kulumba, mkurugenzi katika UBC anayeshuhugulikia masuala ya Qurani na Uislamu amepongeza Kituo cha Utamaduni cha Iran kwa kustawisha utamaduni wa Qurani katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Kwa upande Mohammadreza Qezelsofla, Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Uganda Mohammadreza Qezelsofla amesisitiza ulazima wa kutekeleza kivitendo mafundisho ya Qur'ani.

3977567

 

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* :