IQNA

Iran yaandaa maonyesho ya Qur’ani nchini Uganda

19:44 - April 30, 2021
Habari ID: 3473864
TEHRAN (IQNA) Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Uganda kimeandaa maonyesho ya Qur’ani katika mji wa Kampala kwa mnasaba wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa Shirika la Utamaduni na Mahusiano ya Kiislamu (ICRO), katika maonyesho hayo kumeonyeshwa tarjama za Qur’ani Tukufu kwa luga za Kiingereza, Kifaransa, Kichina na Kiluganda. Aidha kumekuwa na maonyesho ya vitabu vyenye mafundisho ya Qur’ani Tukufu na pia kalamu maalumu za kilektraoniki za kusoma Qur’ani na halikadhalika michoro ya kaligrafia ya Qur’ani Tukufu.

Halikadhalika katika maonyesho hayo kuna program maalumu za kompyuta za kuwafunza watoto Qur’ani Tukufu na halikadhalika vitabu vingi za Kiislamu kwa lugha ya Kiluganda.

3967803

captcha