IQNA

Washindi wa mashindano ya Qur’ani Uganda watunukiwa zawadi

20:12 - May 31, 2021
Habari ID: 3473966
TEHRAN (IQNA)- Washindi wa mashindano ya Qur’ani yaliyofanyika hivi karibuni nchini Uganda wametunukiwa zawadi.

Mashindano hayo yaliandaliwa na Kituo cha Utamaduni cha Iran katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al Mustafa SAW tawi la Kampala.

Mashindano hayo yalikuwa ni ya kusoma, kuhifadi na kutafsiri Qur’ani Tukufu katika kategoria mbali mbali.

Kwa mujibu wa taarifa kulikuwa na nchi 90 ambazo zilishiriki katika mashindano hao ya Qur’ani.

Sherehe ya kuwatunuku zawadi washiriki ilihudhuriwa na Balozi wa Iran nchini Uganda Seyed Hassan Mirhosseini, Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini humo Mohammad Reza Qezelsofla, Naibu Mufti wa Uganda Sheikh Muhammad Ali Waiswa, na mbunge Aisha Kabanda.

Wageni hao wa heshima katika hotuba zao walisisitiza kuhusu Waislamu kunufaika na mafundisho ya Qur’ani Tukufu.

 3974570

captcha