IQNA

Maandamano Kenya kupinga jinai za Wazayuni dhidi ya Wapalestina

19:40 - May 14, 2021
Habari ID: 3473907
TEHRAN (IQNA)- Waislamu nchini Kenya jana waliandamana katika mji mkuu, Nairobi na kubainisha uungaji mkono wao kwa Wapalestina ambao wanakabiliwa na hujuma ya utawala wa Kizayuni wa Israel

Washiriki katika maandamano hayo wamesema mwaka huu wamesherehekea Idi wakiwa katika majonzi kwani Wapalestina wanakabiliwa na mauaji ya umati yanayotekelezwa na wanajeshi wa utawala haramu wa Israel. Akizungumza na Shirika la Habari la Anadolu, mmoja wa washiriki katika maandamano hayo, Hassan Abdi amesema kile kinachofanyika Palestina kinaweza pia kufanyika Kenya na hivyo Wakenya wamejitokeza wakitaka Israel isitishe dhulma dhidi ya Wapalestina.

Naye Ragheb Omar, ambaye ni mfanyabiashara ameliambia shirika hilo la habari kuwa, Idi inapaswa kuwa siku ya furaha lakini Waislamu wa Kenya wana huzuni kwa sababu wenzao wameuawa kinyama na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa upande wake Jacob Njenga, Mkristo aliyeshiriki katika maandamano hayo, amesema kila mwaka Waislamu huwaalika Wakristo katika sherehe za Idi na hivyo anajiunga nao katika kuwaunga mkono Wapalestina ili wapate uhuru.

Polisi mjini Nairobi wametumia gesi ya machozi kuwatawanya Waislamu hao waliokuwa wakiandamana kwa amani. Baadhi ya waandamanaji walikamatwa katika maandamano hayo.

Wakati huo huo, Mufti Wa Uganda Sheikh Shaban Ramadhan Mubajje amelaani mauaji ambayo yametekelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya  Wapalestina katika Msikiti wa Al Aqsa. Kote Uganda, maimamu waliohutubu katika Sala ya Idi walilaani vikali ukatili unaotekelezwa na utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina.

تصاویری از تظاهرات ضدصهیونیستی مردم کنیا

تصاویری از تظاهرات ضدصهیونیستی مردم کنیا

تصاویری از تظاهرات ضدصهیونیستی مردم کنیا

تصاویری از تظاهرات ضدصهیونیستی مردم کنیا

تصاویری از تظاهرات ضدصهیونیستی مردم کنیا

تصاویری از تظاهرات ضدصهیونیستی مردم کنیا

تصاویری از تظاهرات ضدصهیونیستی مردم کنیا

تصاویری از تظاهرات ضدصهیونیستی مردم کنیا

3971475

Kishikizo: kenya palestina israel quds
captcha