IQNA

Maonyesho ya mafanikio ya maisha ya Waislamu Michigan, Marekani

19:42 - July 05, 2021
Habari ID: 3474073
TEHRAN (IQNA)- Maonyesho yanafanyika katika Chuo Kikuu cha Michigano nchini Marekani kwa lengo la kuonyesha maisha ya Waislamu katika maeneo ya Detroit na kusini-mashariki mwa Michigan.

Maoneysho hayo yaliyopewa jina la 'Mji wa Halal' yana michoro ambayo imetayarishwa na Osman Khan na Razi Jafri ambao ni wahadhiri katika chuo hicho. Maoneysho hayo ambayo yataendelea hadi Julai 17 yanaonyesha historia ya Waislamu katika mji wa Detroit katika jimbo la Michigan. Jamii ya Waislamu katika mji wa Detroit imetajwa kuwa yenye mchanganyiko mkubwa zaidi wa Waislamu Marekani.

Waliowasilisha michoro katika maonyesho hayo ni pamoja na  Amna Asghar, Qais Assali, BGIRL MAMA, Nour Ball­out, Adnan Charara, Kecia Escoe, Parisa Ghaderi, Anthony Keith Giannini, Razi Jafri, Osman Khan, Maamoul Press, Endi Poskovic, Haleem “Stringz” Rasul na Reem Taki.

Msikiti wa Dearborn Michigan ni msikiti mkubwa zaidi Amerika ya Kaskazini na ulijengwa takribani miaka 100 iliyopita. Aghalabu ya Waislamu Detroti ni Waarabu lakini kuna makundi mengine ya Waislamu wenye asili ya maeneo mengine dunaini.

 

/3981641

captcha