Hayo yamedokezwa na Meya Mteule wa Michigan, Abdullah Hammoud ambaye amesema kuanzia Januari Mosi Shahin atakuwa kamanda wa polisi katika mji huo na hivyo kumfanya kuwa Muislamu wa kwanza kushika wadhifa huo. Shahin alianza kufanya kazi katika katika Idara ya Polisi ya Dearborn mwaka 1998.
Shahin pia ni mwanachama wa Jumuiya ya Kiislamu ya Amerika Kaskazini na Kamati Dhidi ya Ubaguzi ya Wamarekani- Waarabu.
Naye Hammoud ni Muislamu na Mwarabu-Mmarekani wa kwanza kuwa Meya wa Dearborn. Mji huo ni mashuhuri kwa idadi kubwa ya Waislamu na kwa muda sasa kumekuwa kukitolewa miito ya kutaka idara za serikali ziakisi jamii ya watu wa Dearborn.
Mji wa Dearborn unakadiriwa kuwa na watu 110,000 na ni makao makuu ya shirika kubwa la Marekani la magari, Ford.