Akihutubu baada ya kuapishwa, Hammoud alisema mji wa Dearborn ni kielelezo cha utawala wa wananchi.
Hammoud ni Muislamu na Mwarabu-Mmarekani wa kwanza kuwa Meya wa Dearborn. Mji huo ni mashuhuri kwa idadi kubwa ya Waislamu na kwa muda sasa kumekuwa kukitolewa miito ya kutaka idara za serikali ziakisi jamii ya watu wa Dearborn.
Mji wa Dearborn unakadiriwa kuwa na watu 110,000 na ni makao makuu ya shirika kubwa la Marekani la magari, Ford. Mji huo zamani ulikuwa mashuhuri kwa wabaguzi wa rangi kama vile Orville Hubbard ambaye alikuwa meya aliyetumia maneneo ya matusi dhidi ya Wamarekani Waafrika na Waarabu.
Katika sherehe za kuabishwa Hammoud, viongozi wa kidini wa Madhehebu za Kiislamu za Shia na Sunni pamoja na kasisi Mkristo waliongoza maombi kama njia ya kuonyesha umoja.