IQNA

Ethiopia yapinga hatua ya nchi za Kiarabu kuingilia mgogoro wake na Misri, Sudan

17:52 - July 06, 2021
Habari ID: 3474075
TEHRAN (IQNA)- Serikali ya Ethiopia imepinga vikali uingiliaji wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) mgogoro wake mrefu na Misri pamoja na Sudan kuhusu ujenzi wa bwawa kubwa la maji katika Mto Nile.

Taarifa hiyo ya Jumanne ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia imekuja huku Misri ikilaani hatua ya kuanza tena zoezi la kujaza maji katika bwawa hilo ambalo linajulikana kama An Nahda au Grand Ethiopian Renaissance Dam (GERD). Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kujadili kadhia hiyo Alhamisi.

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imetangaza kuwa unaunga mkono uingiliaji wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa katika mgogoro wa bwawa hilo ingawa Ethiopia inasisitiza kuwa mazungumzo kuhusu mgogoro huyo yafanyike kupitia upatanishi unaoendelea wa Umoja wa Afrika.  Ethiopia imesema Jumuiya ya Nchi za Kiarabu inahistoria ya kupendelea Misri katika mgogoro wa bwawa hilo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Demeke Mekonnen ameliandikia Baraza la Usalama barua kuhusiana na magogoro huo.

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed amesisitiza kuwa hilo litazifaidisha nchi za Ethiopia, Misri na Sudan na litaongeza fursa za amani katika eneo hilo la Afrika.

Abiy Ahmed ambaye alikuwa akihuhutubia kikao cha kufunga Bunge la Ethiopia ameashiria kile alichokielezea kuwa ni nia ya maendeleo na ustawi bara la Afrika na kusema kuwa, nchi yake imeingia katika uwanja wa tasnia ya mvua ya bandia, ambayo itazidisha kiwango cha maji yatakayofika Misri na Sudan.

Bwawa la GERD linajengwa katika Mto Blue Nile nchini Ethiopia na katika umbali wa kilomita 40 katika mpaka wa Sudan. Ethiopia ilianza kujenga bwawa hilo mwezi Apili mwaka 2011 na ujenzi wake unakadiriwa kugharimu dola milioni nne.

3475159

Kishikizo: ethiopia misri sudan bwawa
captcha