IQNA

14:38 - July 09, 2021
News ID: 3474085
TEHRAN (IQNA)- Maelfu ya makaburi ya kale yamegunduliwa mashariki mwa Sudan ambapo yana muundo wa kipekee ambao ulikuwa haujagunduliwa hadi sasa.

Wanaakiolojia wamegundia makaburi hayo yenye muundo wa ajabu unaoshabihiana na kundi la nyota.

Makala iliyochapishwa katika jarida la PLOS One  imesema wanasayansi wametumia picha za satalaiti kugundua karibu makaburi 10,000 huko Kassala mashariki mwa Sudan.

Mtafiti mwandamizi katika mradi huo Stefano Costanzo anasema wanakabiliwa na changamoto ya kubaini maziko yalifanyika vipi katika eneo hilo lakini kilicho wazi ni kuwa mfumo wa mazishi ulikuwa wa aina yake. Anasema mpangilio wa kimahesabu wa makaburi hayo unaashiria maana ya kina katika shughuli hiyo.

Eneo la Kassala Sudan ni la kabila la Beja ambapo aghalabu wanaishi maisha ya kuhamahama na yamkini makaburi hayo yalikuwa ya kikabila na kifamilia.

کشف الگوهای کهکشانی در قبرستان تاریخی اسلامی / آماده

 

کشف الگوهای کهکشانی در قبرستان تاریخی اسلامی / آماده

3982821

Tags: sudan ، kassala ، makaburi
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: