IQNA

Jeshi la Afghanistan lakabiliana na hujuma za Taliban

22:34 - August 01, 2021
Habari ID: 3474148
TEHRAN (IQNA) - Vikosi vya serikali ya Afghanistan vinakabiliana na mashambulio ya Taliban kwenye miji kadhaa mikubwa Jumapili wakati kundi hilo lilizidisha mashambulio ya kitaifa ambayo yalishuhudia uwanja wa ndege muhimu kusini ukishambuliwa kwa maroketi usiku kucha.

Mamia ya makomando walipelekwa katika mji wa magharibi wa Herat wakati wasimamisi katika mji wa kusini wa Lashkar Gah walitaka wanajeshi zaidi kudhibiti mashambulizi hayo.

Mapigano yamezidi nchini kote katika miezi tangu mapema Mei wakati vikosi vamizi vya kigeni vilipoanza kuondoka Afghanistan.

Baada ya kuteka sehemu kubwa za eneo la vijijini na kutekanjia kuu za kuvuka mipaka, Taliban walianza kuzingira miji mikuu ya mkoa.

Safari za ndege kutoka Kandahar, mji wa pili kwa ukubwa nchini Afghanistan na pia ilikuwa ngome ya zamani ya kikundi hicho, zilisitishwa baada ya maroketi kugonga uwanja wa ndege kabla ya alfajiri ya leo.

Mkuu wa uwanja wa ndege Massoud Pashtun alisema roketi mbili ziligonga barabara na ukarabati ulikuwa  ukiendelea na ndege zinaweza kuanza tena huduma baadaye Jumapili.

Vikosi vya usalama vya Afghanistan vimezidi kutegemea mashambulio ya angani kushinikiza wanamgambo kurudi kutoka miji hata wanapokuwa katika hatari ya kupiga raia katika maeneo yenye watu wengi.

Siku ya Jumapili, Wizara ya Ulinzi ilisema kwamba mamia ya makomando walikuwa wametumwa kwa Herat kusaidia kupiga shambulio hilo la waasi.

Hivi karibuni, kundi la wanamgambo wa Taliban lilitoa ujumbe kwa mnasaba wa kuwadia sikukuu ya Idul Adha na kuonyesha hamu na shauku lilionayo ya kupatiwa ufumbuzi matatizo ya Afghanistan kwa njia ya mazungumzo. Mollah Hibatullah Akhundzada mmoja wa viongozi waandamizi wa Taliban amesema katika ujumbe alioutoa kwamba, inasikitisha kuona kuwa upande wa pili (serikali ya Afghanistan) umekuwa ukipoteza fursa hii muhimu. Badala ya kutegemea madola ajinabi, ni bora sisi wenyewe tukayapatia ufumbuzi matatizo ya nchi yetu na kuinasua nchi yetu na kinamasi ilichokwama ndani yake.

Kiongozi huyo wa ngazi za juu wa Taliban sambamba na kukaribisha kwa mikono miwili hatua ya Marekani ya kuondoa majeshi yake nchini Afghanistan amesema kuwa, kundi lao linakaribisha hatua yoyote ile yenye lengo la kudhamani amani na usalama wa nchi hiyo. Hibatullah Akhundzada sanjari na kuashiria hatua iliyopigwa katika mazungumzo ya amani ameeleza kuwa, sisi tukiwa na lengo la kupiga jeki mazungumzo ya amani tumefungua ofisi yetu ya kisiasa huko Qatar na kuteua timu yenye utendaji mzuri kabisa kwa ajili ya mazungumzo ya amani ya Afghanistan.

3475394

Kishikizo: afghanistan taliban
captcha