IQNA

Mtoto mwenye ugonjwa wa tawahudi Oman ahifadhi Qur’ani kikamilifu

19:30 - October 24, 2021
Habari ID: 3474467
TEHRAN (IQNA)- Mvulana mwenye umri wa miaka tisa nchini Oman ambaye anaugua ugonjwa wa tawahudi au autisim ameweza kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu.

Abdul Rahman bin Othman al Abri ambaye anaugua ugonjwa huo wa kijenetiki amejitahidi na hatimaye amefanikiwa kuhifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu..

Ugonjwa wa akili wa watoto au tawahudi ambao unafahamika kwa lugha ya Kiingereza kama autism, ni tatizo la kinafsi na la kihisia.

Wenye tatizo hilo hawaonekani watu wa kawaida. Muda mwingine hawapendi kuangalia wengine pale wanapozungumza nao, au hawapendi kushirikiana na watu wengine katika mambo kadhaa. 

“Tuna furaha kumuenzi Abdul Rahman kutokana na jitihada zake, wazazi na waalimu wake katika kuhifadhi Qur’ani Tukufu,” amesema msemaji wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini Oman.

Mufti Mkuu wa Ufalme wa Oman Sheikh Ahmed bin Hamad Al-Khalili  amemualika mtoto huyo katika ofisi yake na kumuenzi pamoja na wazazi wake kutokana na na mafanikio hayo makubwa.

“Kuhifadhi Qur’ani Tukufu kunahitaji mpango maalumu, ustahamilivu na nidhamu na mvulana huyu ameweza kufanikiwa na hivyo kuushinda ugonjwa wa tawahudi,” amesema Mufti Mkuu wa Oman.

Qur’ani Tukufu ina maneneo 77,797 ambayo yanaunda aya 6,236 na sura 114 na kwa msingi huo kuhifadhi Kitabu hiki kitakatifu si kazi rahisi.

Mwalimu wa Abdul Rahman, Ruqayyah al Abriyah anasema, “ingawa mwanafunzi anaugua tawahudi, hilo halikumzuia kuendelea kuhifadhi Qur’ani Tukufu na ameweza kumaliza kuhifadhi kutokana na motisha na uangalifu wa wazizi wake.”

Mufti Mkuu wa Oman amemshauri mvulana huyo atekeleza mafundisho ya Qur’ani Tukufu katika maisha yake na awe ni kigezo cha kuigwa na watoto wengine wenye matatizo ya kijenetiki duniani kote.

3476173/

captcha