IQNA

Uislamu na Afya

Usonji haujawa kizuizi cha kuhifadhi Qur'ani kwa kijana wa Malaysia

12:40 - September 10, 2024
Habari ID: 3479410
IQNA – Muhammad Naquib Ajmal Mohd Jamal Nasir, mwenye umri wa miaka 26 ambaye aligundulika kuwa na usonji, alihitimu Jumatatu kwa Shahada ya Kwanza ya Mafunzo ya Qur'ani na Sunnah kutoka Universiti Islam Pahang Sultan Ahmad Shah (UNIPSAS).

Licha ya changamoto zinazoletwa na hali yake, Naquib sio tu kwamba alimaliza masomo yake lakini pia alipokea tuzo maalum wakati wa hafla ya 21 ya kongamano la chuo kikuu, Bernama aliripoti.

Akitoa shukrani zake, Naquib alikazia uungwaji mkono wa wazazi na waelimishaji wake kama ufunguo wa mafanikio yake. "Kama sikuwa na usaidizi wao, labda nisingehitimu na kushinda tuzo hii leo... ninashukuru na kushukuru kweli," alisema Naquib, ambaye kwa sasa anahudumu kama mwalimu katika Akademi Syahadah Tahfiz Al-Faizin huko Kuala Selangor.

Katika safari yake yote ya kielimu, Naquib alikabiliwa na matatizo ya kusimamia muda wake kati ya kusoma Qur'ani, tajwiid, na kuhifadhi Qur'ani. Licha ya changamoto hizo, aliendelea kujitolea katika masomo yake na kuhifadhi Qur'ani.

"Ninajitahidi kujifunza kama kila mtu mwingine. Muda ndio kikwazo kikuu cha kusoma huku pia nikishiriki mashindano ya kuhifadhi, lakini najaribu kuandaa na kusawazisha wakati wangu vizuri... Baada ya haya, natamani kushiriki mashindano ya kusoma," Naquib aliongeza na kusisitiza kuendelea kujitolea kwake katika kustawisha  kielimu na kiroho.

Wakitafakari juu ya safari ya mtoto wao, wazazi wa Naquib, Mohammadd Jamal Nasir Ismail na Anita Elias, walikumbuka changamoto za mapema walizokabiliana nazo baada ya kubaini kuwa ana usonji akiwa na umri wa miaka saba.

"Hapo zamani, hakutazama mtu machoni na alikuwa mwepesi wa kuongea; mtoto wangu aliweza tu kuzungumza Kimalei akiwa na umri wa miaka tisa, lakini si kwa ufasaha. Hata hivyo, alijua maneno zaidi ya Kiingereza na Kiarabu," Anita, mwalimu wa Elimu ya Kiislamu, alisimulia.

"Alipokuwa bado mdogo, daktari alituambia kwamba (Muhammad) Naquib alikuwa na kumbukumbu nzuri na anamshukuru Mungu kwa sasa anaweza kuhifadhi Quran," aliongeza, akionyesha shukrani zake kwa kumbukumbu na mafanikio ya mwanawe.

Usonji, ambao pia unajulikana kama  Tawahudi  na Autism kwa Kiingereza, huwatatiza wahusika kwenye masuala ya uhusiano katika jamii,kujieleza na hata kupata marafiki maishani. 

Kutokana na hilo masomo ya kila siku ya kuandika huwakanganya. Hata hivyo ujuzi unaotumia mikono unawasukuma mbele maishani kwani ni werevu. 

3489840

Kishikizo: autism qurani tukufu
captcha