Anaishi katika mji katika Mkoa wa Sohag, kusini mwa Misri. Baada ya baba yake kugundua kipaji chake cha Qur'ani Tukufu, alijaribu kukuza kipaji chake na kumsaidia kuwa qari mashuhuri nchini na ulimwengu wa Kiarabu. Watu katika mji wake wanapenda sauti yake na wanapenda kusikiliza qiraa ya Qur'ani na visomo vya Ibtihal vya kijana huyo.
Marwan ni mfano wa jinsi mtu anavyoweza kufikia malengo yake licha ya magumu na changamoto zote. Anapenda kufanya maendeleo zaidi katika uga wa usomaji wa Qur'ani hadi siku ambapo kisomo chake kinatangazwa kwenye redio. Mafanikio yake yaliangaziwa katika Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu, ambayo huadhimishwa kila mwaka Desemba 3.
Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu ni maadhimisho ya kimataifa yaliyokuzwa na Umoja wa Mataifa tangu 1992. Imeadhimishwa kwa viwango tofauti vya mafanikio kote sayari. Maadhimisho ya Siku hiyo yanalenga kukuza uelewa wa masuala ya ulemavu na kuhamasisha uungwaji mkono kwa ajili ya utu, haki na ustawi wa watu wenye ulemavu. Pia inalenga kuongeza ufahamu wa mafanikio yatakayopatikana kutokana na ushirikiano wa watu wenye ulemavu katika kila nyanja ya maisha ya kisiasa, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni.
Usonji (pia tawahudi, kwa Kiingereza autism) ni tatizo la kinafsi na la kihisia linalowatokea watu tangu utotoni na kuathiri uwezo wao wa kuwasiliana na wengine.
Wenye tatizo hilo hawaonekani watu wa kawaida. Muda mwingine hawapendi kuangalia wengine pale wanapozungumza nao, au hawapendi kushirikiana na watu wengine katika mambo kadhaa. Pia, hawako vizuri katika mawasiliano. Muda mwingine huwa hawawezi kuongea au kuzungumza na watu wengine. Mwishoni, hujijibu wenyewe. Wanaweza wakawa na shauku na kitu ambacho mtu mwingine (ambaye hana tatizo la usonji) hafikirii kina umuhimu.
Uislamu unasisitiz umuhimu wa kuzingatia haki za watu wenye ulemavu.
Quran inasema katika Aya ya 61 ya Suran An-Nur:
“Si vibaya kwa kipofu, wala si vibaya kwa kiguru, wala si vibaya kwa mgonjwa, wala kwenu nyinyi, mkila katika nyumba zenu, au nyumba za baba zenu, au nyumba za mama zenu, au nyumba za kaka zenu, au nyumba za dada zenu, au nyumba za ami zenu, au nyumba za shangazi zenu, au nyumba za wajomba zenu, au nyumba za dada wa mama zenu, au za mlio washikia funguo zao, au rafiki yenu. Si vibaya kwenu mkila pamoja au mbali mbali. Na mkiingia katika nyumba, toleaneni salamu, kuwa ni maamkio yanayo toka kwa Mwenyezi Mungu, yenye baraka na mema. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo kubainishieni Aya zake mpate kuelewa.”
Ulemavu ni kizuizi lakini haimaanishi kutokuwa na uwezo. Qur'an Tukufu inasema kuwa kuwepo kwa matatizo na upungufu katika maisha ni mtihani wa Mwenyezi Mungu kwa watu. Kwa mujibu wa Aya ya 155-156 ya Surah Al-Baqarah, *Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri: ‘Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea..
Ifuatayo ni kisomo cha Kurani cha Marwan Abdul Ghani:
4251860