IQNA

Hamas, Jihad Islami zaionya Israel kuhusu mateka Wapalestina

18:49 - November 03, 2021
Habari ID: 3474509
TEHRAN (IQNA)- Harakati za kupigania ukombozi wa Wapalestina za Hamas na Jihad Islami zimetoa tahadhari kwa utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu kuwatesa mateka Wapalestina wanaoshikiliwa na utawala huo dhalimu.

Hamas na Jihad Islami zimeuonya vikali utawala wa Kizayuni kuwa iwapo hautasitisha ukandamizaji wa mateka Wapalestina katika jela za kuogofya za utawala  huo, hasa iwapo mateka watakufa shahidi, basi hali itakuwa mbaya sana.

Mohammed Shalah, mmoja wa viongozi waandamizi wa Jihad Islami ya Palestina ameiambia televisheni ya al-Mayadeen ya Lebanon kuwa, "tunasimama kidete na wafungwa wa Kipalestina na tunauonya utawala ghasibu wa Israel usijidhuru."

Ameeleza bayana kuwa, iwapo mfungwa yeyote wa Palestina ataaga dunia kutokana na hali mbaya katika jela na magereza na Israel, basi harakati hiyo haitakuwa na chaguo jingine isipokuwa kuanzisha vita vya wazi vya silaha na Wazayuni.

Shalah amesisitiza kuwa: Tutawalinda mateka wote kwa njia zote, machaguo yote yapo mezani. Kufa shahidi mfungwa yeyote kutachochea hali ambayo haitamsaza yeyote. Kambi ya muqawama itachukua hatua za kuwalinda wafungwa wa Palestina.

Katikati ya mwezi uliopita wa Oktoba, harakati hiyo ya muqawama ilitangaza kuwa, mateka 150 wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika magereza za Israel wameanza mgomo wa kula.

Jihad Islami imewataka wapenda haki wote duniani kupaza sauti ya kuwatetea maelfu ya mateka wa Kipalestina wanaoishi katika mazingira mabaya kwenye jela na magereza ya Israel.

Wapalestina karibu elfu 4 na 800 wanashikiliwa katika korokoro za kutisha za utawala haramu wa Israel wakiwemo watoto wadogo 170.   

4010309/

captcha