IQNA

18:58 - October 25, 2021
News ID: 3474471
TEHRAN (IQNA)- Utawala wa Kizayuni wa Israel umewakamata Wapalestina zaidi ya 1,280 katika kipindi cha miezi mitati iliyopita.

Hayo yamo kwenye ripoti ya pamoja na mashirika kadhaa ya haki za binadamu Palestina.

Ripoti hiyo imetolewa na Shirika la Haki za Binadamu la Addameer, Tume ya PLO ya Wafungwa na Wafungwa Walioachiliwa Huru, Jumuiya ya Wafungwa Wapalestina na Kituo cha Habari cha Wadi Al Hilwah.

Kwa mujibu wa mashirika hayo, ripoti hiyo inajumuisha kipindi cha kuanzia Julai hadi Septemba 2021 ambapo watu 525 walikamatwa katika mji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu.

Karibu watoto 160 na wanawake 37 ni miongoni mwa waliokamatwa.

Ripoti hiyo imebaini kuwa kwa ujumla hadi kufikia mwezi Septemba kulikuwa na wafungwa au mateka 4,600 katika jela za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel na miongoni mwao kuna wanawake 35 na watoto 200.

Hivi karibuni Harakati ya Jihad Islami ya Palestina imetangaza kuwa, mateka 150 wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika magereza za Israel walianza mgomo wa kula tangu jana Jumatano.

Msemaji wa Jihad Islami, Tariq Izzuddin amesema kuwa, kuanza mgomo huo wa matekani wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika magereza na jela za Israel ni hatua muhimu katika vita vya Wapalestina hao dhidi ya mamlaka za magereza za Israel na taasisi za ujasusi za utawala huo.

Izzuddin ameongeza kuwa kuwatetea matekani ni wadhifa mtakatifu wa kitaifa na kusema kuwa, hatua zote za maandamano, mihadhara na harakati za aina tofauti ni huduma muhimu katika kupaza sauti ya kuwatetea mateka hao wanaokumbana na mashaka na manyanyaso makubwa. 

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: