Wizara ya Wakfu Misri imetangaza kuwa, vituo hivyo vitaanza kazi Disemba 1 sambamba na vituo vyote vya utamaduni kote Misri.
Wizara hiyo imesema vituo hivyo vina nafasi muhimu katika kuwapa mafunzo waalimu ambao wanaeneza misimamo ya wastani ya Uislamu na kurekebisha itikadi potovu. Vituo hivyo pia vinastawisha utamaduni wa kuhifadhi Qur'ani.
Vituo vyote vya kufunzwa Qur'ani Misri, sawa na taasisi zingine za kidini, kielimu na kiutamaduni, zilifungwa mwaka jana ili kuzuia maambukizi ya COVID-19. Hadi sasa watu 347,000 wameambukizwa COVID-19 nchini Misri huku wengine 19,000 wakipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo nchini humo.