IQNA

Sala ya Ijumaa yaanza tena Brunei baada ya miezi mitatu

13:22 - November 20, 2021
Habari ID: 3474580
TEHRAN (IQNA)- Sala ya Ijumaa imeruhusiwa tena nchini Brunei baada ya kusitishwa kwa muda wa miezi mitatu.

Waislamu waliweza kuswali tena Sala ya Ijumaa jana kote Brunei huku wakitakiwa kuzingatia kanuni za kiafya za kuzuia kuenea COVID-19 kama vile kutokaribiana.

Hivi sasa pia misikiti inaruhusiwa kuwa na sala tano za kila siku kama sehemu ya mpito kuelekea hali ya kawaida baada ya shughuli nyingi kufungwa nchini humo kuzuia kuenea COVID-19.

Walioshiriki katika Sala ya Ijumaa walionekana wakiwa wamevaa barakoa huku wakikaguliwa kupitia mfumo maalumu wa BruHealth kubaini iwapo wamepata chanjo ya COVID-19.

Askari wa Jeshi la Brunei walishirikiana na polisi pamoja na kamati za misikiti walishirikiana kusimamia utaratibu wa waumini kuingia na kutoka misikitini.

/347655

Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha