IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani ya Brunei kuanza Jumatano

17:13 - January 16, 2024
Habari ID: 3478200
IQNA - Mashindano ya kitaifa ya Qur'ani Tukufu ya Brunei yataanza Jumatano, Januari 17.

Duru ya awali ya Ngazi ya Kitaifa ya Kuhifadhi Qur'ani Tukufu na Mashindano Uelewa kwa mwaka wa kalenda ya 1445 Hijri itafanyika kwa siku sita, yaani  Januari 17, 18, 20, 22, 23 na 24.
Kituo cha Mafunzo na Usambazaji wa Al-Quran MABIMS katika mji mkuu,Bandar Seri Begawan, kitaandaa hafla hiyo, Wizara ya Masuala ya Kidini ya nchi hiyo ilisema katika taarifa yake Jumatatu.
Kitengo cha ‘A’ kitafanyika Januari 17, huku Kitengo ‘B’ Januari 18, Kitengo ‘C’ Januari 23 na 24, Kitengo ‘D’ Januari 20 na Kitengo ‘E’ kikifanyika Januari 22.
Brunei ni nchi huru lililoko kwenye pwani ya kaskazini ya kisiwa cha Borneo huko Kusini-mashariki mwa Asia.
Uislamu ni dini rasmi ya Brunei na karibu asilimia 70 ya wakazi ni Waislamu.

3486828

captcha