IQNA

Harakati za Qur'ani

Brunei: Waliosilimu wapewa vyetu baada ya kumaliza kozi ya Qur'ani

15:14 - September 22, 2024
Habari ID: 3479466
IQNA - Programu ya siku nne ya Al-Quran kwa waliosilimu ilihitimishwa kwa hafla ya kutunukiwa washiriki wa kozi hiyo katika Kituo cha Da'wah cha Kiislamu (PDI) siku ya Jumamosi.

Kozi hiyo iliyoanza Septemba 17, iliandaliwa na Kituo cha Utafiti na Usambazaji cha MABIMS Al-Quran, Wizara ya Masuala ya Kidini, kwa ushirikiano na PDI.

Jumla ya watu 56 ambao wamesilimu na hivyo kuukumbatia Uislamu kama njia ya maisha walishiriki katika mpango huo. Mada zilizojadiliwa ni pamoja na dhana ya ibada na uhusiano wake kati ya Khaliq (Allah/Muumba) na viumbe; umuhimu na nafasi ya swala katika maisha ya Kiislamu; saumu na athari zake katika malezi ya shakhsia ya Kiislamu; na Zaka na nafasi yake katika maendeleo ya kijamii na pia safari ya Hija.

Mpango huo pia umesisitiza msimamo wa Qur'ani Tukufu kuwa ndio chanzo kikuu cha sheria za Kiislamu, unaolenga kuongeza uelewa wa Qur'ani katika nyanja mbalimbali na kufafanua dhana potofu.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Masuala ya Dini, Haji Mohammad Rosli bin Haji Ibrahim.

3489985

Kishikizo: brunei qurani tukufu
captcha