IQNA

Watoto 300 wa Yemen wanapoteza vita kila siku kutokana na vita vya Saudia

16:42 - November 21, 2021
Habari ID: 3474584
TEHRAN (IQNA)- Shirika moja la kutetea haki za binadamu limesema mamia ya watoto wa Yemen wanafariki dunia ndani ya kila saa 24 kutokana na utapiamlo, huku muungano wa kivita unaoongozwa na Saudi Arabia ukiendelea kufanya mashambulizi na kuliwewekea mzingiro wa kila upande taifa hilo maskini la Kiarabu.

Kwa mujibu wa Shirika la Entesaf la Kupigania Haki za Wanawake na Watoto lenye makao yake nchini Yemen, watoto zaidi ya 300 wa Kiyemen wanaaga dunia kila siku kutokana na utapiamlo wa kiwango cha juu.

Ripoti ya shirika hilo iliyotolewa jana Alkhamisi mjini Sana'a imeongeza kuwa, watoto 3,825 wa Yemen wameaga dunia, huku wengine zaidi ya 4,157 wakijeruhiwa tangu Saudia iivamie nchi hiyo jirani yake miaka sita iliyopita.

Ripoti ya shirika la Entesaf imebainisha kuwa, watoto zaidi ya 3000 wa Yemen wanasumbuliwa na magojwa sugu tangu kuzaliwa kwao, huku wengine wapatao 3000 wakihitaji kufanyiwa upasuaji wa moyo nje ya nchi hiyo haraka iwezekanavyo.

Mwaka jana, Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu Yemen, Lise Grande alionya kwamba, ikiwa vita havitomalizwa katika taifa hilo, basi Yemen itaelekea kwenye hali ambayo haitoweza kubadilishwa na kuingia kwenye hatari ya kupoteza kizazi kizima cha watoto nchini humo.

Kufuatia uungaji mkono wa Marekani, Imarati, utawala haramu wa Israel na nchi nyingine kadhaa za Kiarabu, Saudi Arabia iliivamia kijeshi nchi masikini ya Yemen mnamo Machi 2015 na kuiwekea mzingiro wa pande zote wa nchi kavu, anga na majini. Uvamizi wa kijeshi wa Saudia umeisababishia pia nchi masikini ya Yemen uhaba mkubwa wa chakula na dawa.

/3476573/

captcha