IQNA

Jamii ya kimataifa yalaumiwa kwa kunyamazia kimya jinai za Saudia nchini Yemen

22:53 - December 25, 2021
Habari ID: 3474722
TEHRAN (IQNA)- Msemaji wa serikali ya uwokovu wa kitaifa ya Yemen amekosoa kimya cha jamii ya kimataifa kwa jinai zinazofanywa na muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya watu wa Yemen na akasema, kuendelea kwa jinai hizo hakutakuwa na matokeo mengine isipokuwa wavamizi hao kufikwa na mwisho mbaya.

Muhammad Abdussalam ametoa kauli hiyo kufuatia jinai za jana usiku zilizofanywa na muungano vamizi wa Saudia katika mkoa wa Al Mahwit na akaeleza kwamba, kwa kujinufaisha na uungaji mkono wa jamii ya kimataifa na kimya cha Umoja wa Mataifa, muungano huo vamizi unaendeleza mashambulio yake dhidi ya raia na maeneo yasiyo ya kijeshi nchini Yemen.

Abdussalam ameongeza kuwa, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kuendelea kwa jinai hizo hakutakuwa na matokeo mengine kwa muungano vamizi wa Kisaudi na Kimarekani ghairi ya kufikwa na mwisho mbaya na adhabu.

Duru za Yemen ziliripoti jana usiku kuwa, ndege za kivita za Saudia zimeshambulia mkoa wa Al Mahwit na kuwaua shahidi na kuwajeruhi raia 10 wakiwemo wanawake wawili na mtoto mdogo mmoja.

Moto wa vita uliowashwa na Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya Yemen kuanzia Machi 2015 na kuendelea hadi sasa umeshapelekea mamia ya maelfu ya watu wasio na hatia kupoteza maisha, mbali na kuwaacha wengine milioni nne wakiwa hawana pa kuishi.

Uchokozi na uvamzi wa kijeshi wa Sadia dhidi ya Yemen umebomoa na kuharibu zaidi ya asilimia 85 ya miundombinu ya nchi hiyo masikini zaidi katika Bara Arabu na kuisababishia pia uhaba mkubwa wa chakula na dawa.

3477083

Kishikizo: yemen saudia
captcha