IQNA

Wamisri washiriki katika Sala ya Kuomba Mvua

13:56 - November 22, 2021
Habari ID: 3474589
TEHRAN (IQNA) –Waislamu kote nchini Misri wameshiriki katika Sala ya Istisqa yaani Sala ya Kuomba Mvua.

Sala hiyo imesaliwa Jumapili katika misikiti ya miji mikubwa na midogo na vijiji kote katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Mapema Sheikh Mohamed Mokhtar Gomaa Waziri wa Wakfu wa Misri alikuwa amewaomba watu wa nchi hiyo washiriki katika Sala ya Istisqaa kumuomba Mwenyezi Mungu aitunuku nchi hiyo kwa Baraka ya mvua kufuatia kiangazi cha muda mrefu.

Istisqaa ni sala maalumu ya kuomba mvua wakati nchi inapokumbwa na kiangazia au mvua duni.

Hivi karibuni Waislamu katika nchi nyingi za eneo la Asia Magharibi au Mashariki ya Kati wameshiriki katika Sala ya Istisqaa. Saudi Arabia, Qatar, Jordan na Umoja wa Falme za Kiarabu ni kati ya nchi ambazo waumini wameshashiri katika Sala ya kuomba mvua.  

4015044

captcha