IQNA

Kiangazi duniani

Sala ya Istisqa (ya kuomba mvua) kusaliwa kote UAE

18:47 - November 08, 2022
Habari ID: 3476057
TEHRAN (IQNA) – Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ametoa wito kwa wauminikuhudhuria sala ya Istisqa siku ya Ijumaa, Novemba 11.

Katika taarifa yake siku ya Jumapili, Mohamed bin Zayed Al Nahyan alitoa wito wa kufanyika kwa Sala ya Istisqa kote nchini humi. Sala hiyo maalum itasaliwa katika misikiti kote UAE saa tano unusu machana  kwa saa za nchi hiyo ya Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi.

Sala ya Istisqa ni  Sala maalumu ya Kiislamu ya kumuomba Mwenyezi Mungu ateremshe mvua ya neema na huombwa wakati wa ukame au mvua zinapopungua.

Kwa mujibu wa riwaya, Mtume Muhammad (SAW) alisali Sala ya Istisqa katika uwanja na ni sala ya rakaa mbilii.

Salatul-Istisqa inajuzu kunapokuwa na ukame na mvua chache, au kiwango cha maji katika mito na kisima kikiwa kidogo, au kutokana na mto kukauka.

3481161

Kishikizo: sala ya istisqa mvua
captcha