IQNA

Kikao cha mazungumzo ya kidini baina ya Al Azhar na Vatican

15:16 - December 06, 2021
Habari ID: 3474645
TEHRAN (IQNA)- Chuo cha Kiislamu cha Al Azhar kimefanya kikao cha mazungumzo ya kidini na Makao ya Kanisa Katoliki Duniani, Vatican na Kanisa la Orthodox la Koptiki.

Kikao hicho ambacho kimefanyika chini ya anuani ya 'Matunda ya Mazungumzo baina ya Vatican na Al Azhar Kuhusu Udugu wa Kibinadamu', yamefanyika kwa uwenyeji wa Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar.

Akizungumza katika kikao hicho, Nazeer Ayad, Katibu Mkuu wa Akademia ya Utafiti wa Kiislamu katika Chuo cha Al Azhar amesema msingi wa mafundisho ya Kiislamu ni kustahamiliana na kuishi kwa maelewano wafuasi wa mataifa, staarabu na tamaduni mbali mbali bila kujali rangi au kaumu.

Amesema mafundisho ya Kiislamu yanasisitiza kuheshimiana wafuasi wa dini mbali mbali kwani hilo litakuwa chimbuko wa ustaarabu wa kupendana na kuheshimiana katika nyoyo za watu.

Huku akiashiria umuhimu wa mazungumzo baina ya wafuasi wa dini mbali mbali, Ayad amesema vikao kama hivyo hudhamini uhuru wa dini na imani katika dunia iliyojaa malumbano na ukosefu wa uadilifu sambamba na baadhi ya makundi kujaribu kutumia vibaya kadhia ya itikadi.

Amesema Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar kikiko mbinu kuandika rasimu ya udugu wa kibinadamu na tayari vikao kadhaa vya kimataifa vinafanyika kuarifisha rasimu hiyo.

Mkutano huo wa Cairo ulihudhuriwa na Rais wa Chuo Kikuu cha Al Azhar Profesa Mohamed Al-Mahrasawy, Rais wa Baraza la Vatican la Mazungumzo Baina ya Dini Kadinali Miguel Angel Ayuso Guixot na Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Kanisa la Orthodox la Koptiki.

4018686

captcha