IQNA

Watetezi wa Palestina

Mwanazuoni wa Kiislamu Iraq atetea Palestina katika mkutano na ujumbe wa Vatican

16:26 - December 06, 2023
Habari ID: 3477995
KARBALA (IQNA) - Sheikh Abdul Mahdi al-Karbalayi, mwakilishi wa Ayatullah Sayyed Ali al-Sistani jijini Karbala, Iraq amesisitiza uungaji mkono kwa watu wa Palestina katika kukabiliana na uchokozi wa kikatili wa utawala wa Kizayuni.

Sheikh al-Karbalayi alisema hayo wakati wa mkutano na ujumbe kutoka Vatican na kuongeza kuwa: "Tunasimama pamoja na wanyonge popote walipo duniani, wakiwemo Wapalestina ambao wanakabiliwa na ukandamizaji na mauaji ya halaiki."

Alisikitishwa na kampeni ya Israel ya kuendelea kuua raia katika Ukanda wa Gaza, akibainisha kwamba maelfu wamepoteza maisha huko Gaza, asilimia 70 kati yao wakiwa wanawake na watoto.

Mwanazuoni  huyo wa ngazi za juu alisisitiza kwamba kanuni za kibinadamu zinahitaji kuunga mkono na Wapalestina wanaodhulumiwa.

Aidha amewataka wajumbe wa Vatican kufikisha salamu zake kwa Baba Mtakatifu Francisko.

Ujumbe huo, ukiongozwa na mwakilishi wa Papa, ulimtembelea Sheikh al-Karbalayi, ambaye amefanyiwa upasuaji, nyumbani kwake huko Karbala.

Zaidi ya Wapalestina 16,000 wameuawa na utawala wa Israel huko Gaza tangu ulipoanzisha mashambulizi yake mabaya kwenye eneo la pwani Oktoba 7.

Takriban miezi miwili baada ya mashambulizi ya umwagaji damu ya Israel, utawala huo ghasibu unafanya uharibifu katika kila kona ya ardhi ya Gaza na kuacha njia ya vifo na uharibifu pia ukikata mojawapo ya maeneo yenye wakazi wengi zaidi duniani kutoka na vifaa vya msingi kama vile maji, umeme, dawa, na mafuta na kuacha mamilioni ya Wapalestina katika hatari ya njaa.

3486313

captcha