IQNA

Wito wa Vatican na Al-Azhar wa kuwepo siku ya pamoja ya duaa

14:55 - May 04, 2020
Habari ID: 3472733
TEHRAN (IQNA) - Baraza kuu la kutekeleza malengo ya Waraka wa Urafiki wa Kibinadamu baina ya Taasisi ya Al-Azhar ya Misri na Vatican limetoa wito kwa viongozi na wafuasi wa dini zote duniani kuainisha Mei 14 kama siku maalumu ya duaa na maombi kwa ajili ya kumuomba Mwenyezi Mungu ainusuru dunia kutokana na janga la COVID-19.

Katika taarifa ya pamoja, taasisi hizo mbili muhimu za Kiislamu na Kikristo zimetoa wito kwa watu wote duniani kumuomba Mwenyezi Mungu aondoe janga la ugonjwa wa COVID-19 au corona na awasaidie wanasayansi kupata tiba ya ugonjwa huo.
Mnamo Februari 2019, Imam Mkuu wa Al Azhar Sheikh Ahmad el-Tayeb na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francisi walitia saini waraka Waraka wa Urafiki wa Kibinadamu .
Wakati wa kuanza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Papa Francis alimtumia salamu za kheria na fanaka Imam Mkuu wa Al Azhar na wawili hao walijadili pia njia za kuimarisha mshikamano wa dunia katika kukabiliana na janga la COVID-19.

3896233

captcha