IQNA

Nakala za kale za Qur'ani zilizoko Vatican

17:37 - August 31, 2025
Habari ID: 3481164
IQNA – Ingawa Maktaba ya Vatican ni maktaba ya Kikristo, urithi wa Kiislamu unachukua nafasi maalum ndani yake na Misahafu (nakala za Qur'ani) inahifadhiwa katika maktaba hii.

Kulingana na ripoti ya Al Arabiya, kwa karne nyingi, hati za Kiarabu zimefika kwa njia mbalimbali duniani kote, hadi kufikia hatua ambapo hakuna maktaba yoyote katika miji mikuu ya dunia isiyo na sehemu ya hazina ya urithi wa Kiarabu na Kiislamu. Kwa njia hii, hati za Kiarabu zimeeneza maarifa mengi katika lugha mbalimbali kwa njia isiyokuwa na kifani.

Italia, kama vile nchi nyingine za Magharibi, imepokea sehemu kubwa ya utajiri huu. Mkusanyiko wa kwanza wa hati za Mashariki uliwasilishwa na Baraza la Florence mnamo mwaka 1441 na Maktaba ya Vatican iliyopo Roma. Hati hizi za Kiarabu za kidini zililetwa na wahadhiri wa Mashariki waliotoka Alexandria na Quds (Jerusalemu) ili kushiriki katika mikutano ya baraza hilo.

Kisha, kwa ufunguzi wa Nyumba ya Uchapishaji ya Medici huko Florence (1584), hati za Kiarabu ziliiendelea kuongezeka. Kulingana na mwandishi wa kitabu "Njia ya Herufi" (2012), hati za kwanza za Kiarabu zilizopatikana na nyumba hii ya uchapishaji zilikuwa kutoka kwa  Patriarki wa Syriac, Athanasius Nematullah (aliye fariki 1587), kuhusu siri za ulimwengu, sayansi ya nyota, na unajimu.

Hati za Kiarabu kutoka Yemen

Idadi ya vitabu au hati za Kiarabu kutoka nchini Italia inakadiriwa kuwa 3,300. Giuseppe Caprotti alikuwa na nafasi kubwa katika kuhamasisha vitabu vya Kiarabu kutoka Yemen kuingizwaItalia.

Valentina Rossi anaandika katika kitabu chake "Maandiko ya Italia" kwamba Caprotti alifika katika mji wa Al-Hodeidah nchini Yemen mnamo mwaka 1885 na kisha akaenda kukaa Sanaa. Aliishi huko kwa takribani miongo mitatu na wakati huu aliweza kukusanya hati na vitabu vingi vya Yemen na kwa siri kuvipeleka Milan, Italia. Shehena hii ilikuwa na karibu masanduku 60 yaliyojaa vitabu na makala zenye hatia za Kiarabu ambapo kulikuwa na jumla ya zaidi ya vitabu 1,800.

Hadi mwaka 1909, maandiko 1,610 ya Kiarabu kutoka kwa mkusanyiko wa Caprotti yalihamishiwa katika Maktaba ya Ambrosiana huko Milan, na mnamo mwaka 1914, maandiko mengine 250 kutoka kwa mkusanyiko huu yalihamishiwa kwenye maktaba hii na Seneta Luca Beltrami. Hivyo, Maktaba ya Ambrosiana ilikusanya maandiko 2,040, mengi yakiletwa kutoka Rasi ya Kiarabu ya Kusini.

Maktaba ya Vatican

Maktaba ya Vatican ni mojawapo ya hazina za siri na thamani ya kipekee ya maarifa ya wanadamu; ni sehemu ambayo haiwezi kufikiwa na umma, lakini thamani yake ya kitamaduni na kihistoria ni kubwa kupita maelezo. Jengo la kifahari lenye maandiko elfu kadhaa, hati za kihistoria na vitabu vya thamani, baadhi ya ambavyo vinatoka miaka mingi iliyopita.

Maktaba ya Vatican, inayojulikana kama VAT, ilianzishwa rasmi mwaka 1475. Maktaba hii ina vitabu takriban 75,000 na nakala 85,000 za vitabu vya uchapishaji wa awali, yaani vitabu vilivyochapishwa tangu uvumbuzi wa uchapishaji katikati ya karne ya 15 hadi karne ya 16, na inajumuisha zaidi ya vitabu milioni moja.

Maktaba hii ina maandiko 2,217 ya Kiarabu, bila kuhesabu maandiko ya Kiarabu ya Kikristo.

Maktaba ya Ambrosiana

Maktaba hii iko Milan, Italia na ni ya pili kwa ukubwa baada ya Maktaba ya Vatican kwa vitabu vya hati za Kiarabu, ikiwa na vitabu 2,040 ya Kiarabu.

Maktaba ya Chuo Kikuu cha Linz

Maktaba ya Linz huko Roma ina hazina ya vitaby vya kipekee vya Kiarabu , ambayo, kulingana na orodha ya maandiko, inajumuisha vitabu 82 vya Kiarabu. Pia, vitabu vipya  75 vimeongezwa hivi karibuni, ambapo 63 kati yake ni vitabu ya Kiyemeni.

Nakala za Qur’ani katika Maktaba ya Vatican

Ingawa Maktaba ya Vatican ni maktaba ya Kikristo, urithi wa Kiislamu unachukua nafasi maalum ndani yake. Miongoni mwa urithi huu, nakala nyingi za Qur'ani zinahifadhiwa katika maktaba hii, lakini nyingi ni sehemu za Qur’an na si Qur’an kamili, kutoka Surah Al-Fatiha hadi Surah An-Nas.

Hati za nakala za Qur’ani katika Maktaba ya Vatican zinachukuliwa kuwa vitabu vya thamani na vya kipekee, na idadi yake inafikia nakala 144 kwa vipengele mbalimbali. Hii ni ikilinganishwa na nakala 71 za Qur’an zilizopo katika maktaba nyingine za Roma.

Nakala za Qur’an kutoka Morocco, Afrika ya Kusini mwa Sahara, Mashariki ya Kiarabu, Dola la Uthmaniya, Iran, na India zimefika katika maktaba hii, ambapo ya muhimu zaidi ni Misahafu kutoka Morocco.

Kinachotofautisha Misahafu ya Morocco ni kwamba ni ya kifahari, iliyoandikwa kwa ustadi mkubwa, na mara nyingi imeandikwa kwenye karatasi. Kuna mkusanyiko wa Morocco ulioandikwa kwenye karatasi unaorudi nyuma hadi mwaka 1488, uliochapishwa katika Msikiti Mkuu wa Zeitouna nchini Tunisia. Nakala hii inajulikana kwa ukubwa wake mkubwa na ubora wa juu.

Miongoni mwa hati hizi, kuna nakala ya Qur’ani inayojitokeza kutoka kwa mengine kwa sababu kurasa zake mbili za mwanzo zina mapambo mazuri na michoro. Msahafu huu umeandikwa kwa maandishi ya Naskh, lakini mwandishi wake na wakati wa kuandika haijulikani.

Mkusanyiko wa pili wa maandiko unajumuisha nakala ya Qur’an kutoka kipindi cha Uthmaniya, idadi yake katika maktaba za Roma ikiwa nakala 157. Mkusanyiko huu unaunda sehemu kubwa ya nakala za Qur’ani kwa idadi, na kipengele cha jumla kinachotofautisha mkusanyiko huu na Qur’ani nyingine ni kwamba ni maalum na ya kati kwa ukubwa.

Mkusanyiko wa tatu wa Misahafu kutoka vyanzo mbalimbali umehamishiwa kwenye maktaba za Roma. Hizi ni pamoja na: nakala 12 kutoka nchi za Mashariki, 12 kutoka Iran, 4 kutoka nchi za Afrika ya Kusini mwa Sahara yaliyoandikwa kwa maandishi ya Kimaroko. Aidha, miongoni mwa mkusanyiko wa Maktaba ya Vatican, kuna nakala  ya Qur’an iliyoandikwa kwa herufi za Kiebrania.

Nakala hii ni ya Giovanni Pico della Mirandola na ni yamwanzoni mwa karne ya 15.

Hati zingine katika Maktaba ya Vatican

Hadithi za Mtume Muhammad (SAW): Huu ni mkusanyiko wa maandiko ya Andalusia unaojumuisha hadithi za Mtume (SAW) na inaonekana kuwa ilikuwa ni kitabu cha masomo. Pia, kwenye ukurasa wa kichwa imeandikwa kwamba kitabu hiki kilitolewa kwa ajili ya shule ya Granada (nchini Hispania).

Al-Anwar al-Muhammadiyah: Huu ni mkusanyiko wa hati za Kiarabu kutoka kwa Abu al-Hasan Abdullah al-Bakri, lakini mwandishi wake na wakati na mahali pa kuandika haijulikani.

Jawaher al-Quran wa Durarah: Huu ni mkusanyiko wa hati za Kiarabu kutoka kwa Abu Hamid al-Ghazali, lakini mwandishi wa kitabu hiki hakutoa taarifa kuhusu wakati na mahali pa kuandika wala jina lake.

Al-Kafi fi al-Fiqh: Huu ni kitabu kutoka kwa Abu Omar bin Abdullah bin Muhammad bin Abdulbar al-Numiri, kilichoandikwa kuhusu fiqhi ya shule ya Malik bin Anas, miongoni mwa maimamu wa Ahul Sunna, na kinajumuisha sura kadhaa, ikiwa ni pamoja na: kitabu cha sala, kitabu cha wudhu, kitabu cha zaka, n.k.

Mwisho wa kitabu hiki kuna maandiko yafuatayo: "Kitabu cha Al-Kafi kiliandikwa, kwa msaada wa Mungu, katika siku kumi za mwanzo za mwezi wa Sha’ban, 849 AH, kwa mkono wa mtumishi anayeihitaji rehema za Mungu, Abu al-Khalil Ibrahim al-Qalbi, mhubiri wa Msikiti Mkuu wa jiji la Tarazuna (nchini Hispania)."

Hadithi za Mitume: Huu ni mkusanyiko wa hati za Kiarabu wenye sura 5 na unajumuisha hadithi za maisha ya mitume, kuanzia kwa Ismaili (AS) na watoto wake, kisha hadi hadithi ya maisha ya Mtume Muhammad (PBUH) na kutajwa kwa jina lake katika Torati na vitabu vya mitume (AS).

3494430

captcha